Loading...

Fatma Karume amrithi Tundu Lissu TLS


Wakili Msomi Fatma Karume ameshinda nafasi ya Urais wa Chama Cha Mawakili wa Tanganyika (TLS) na kuwa mrithi wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu ambaye amemaliza muda wake leo kutumikia nafasi hiyo kama Rais.

Fatma Karume ametangazwa mshindi baada ya kuwashinda Simba Ngwilimi, Musa Mwapongo pamoja na Godfrey Wasonga ambao nao walikuwa wakigombea nafasi hiyo ya Urais wa TLS.

Kufuatia ushindi huo wa Fatma Karume Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameweza kuwatumia ujumbe wa pongenzi na kusema kuwa wao watashirikiana nao kuhakikisha utawala wa sheria na Katiba unafuatwa nchini.

"Nawapongeza sana Fatma Karume na Dkt. Rugemeleza Nshala kwa kuchaguliwa kuwa Rais na Makamu wa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika ( TLS ). Ushindi wenu ni ushahidi wa imani kubwa waliyonayo wanasheria nchini. Tutashirikiana Katika kuhakikisha utawala wa sheria na Katiba unafuatwa nchini" alisisitiza Zitto Kabwe
Fatma Karume amrithi Tundu Lissu TLS Fatma Karume amrithi Tundu Lissu TLS Reviewed by Zero Degree on 4/14/2018 02:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.