Loading...

PSG inaweza kumsajili nyota huyu wa Real Madrid

Paris Saint-Germain wanaweza kugeukia kwa mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema
Karim Benzama ana msimu mzuri katika klabu ya Real Madrid. Mkufuzi wa klabu hiyo, Zinedine Zidane alimpa nafasi Mfaransa huyo kuonyesha thamani lakini alishindwa. Amefunga magoli 8 katika mechi 34, ikiwa ni hesabu yake mbaya ya kwanza tangu ajiunge na Madrid mwaka 2009.
Mshambuliaji huyo aliachwa nje kwenye robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Juventus. Rais wa Real Madrid, Florentino Perez tayari ana mpango wa kusajili mshambuliaji mwingine kwenye majira ya joto, inaaminika kuwa muda wa Mfaransa huyo katika klabu hiyo umeisha.

Kulingana na taarifa za nchini Ufaransa, Paris Saint-Germain wanaweza kugeukia kwa mshambuliaji huyo kwenye majira ya joto.
PSG pia inatarajiwa kuwa na mambo mengi ya kufanya wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa. Unai Emery anatarajiwa kuondoka mwishoni mwa msimu baada ya kufanya vibaya kwenye Ligi ya Mabingwa na wachezaji wachache pia wanatarajiwa kuondoka. Mmoja wa wachezaji anaweza kuwa Edison Cavani, ambaye amekuwa na wakati mgumu tangu kuwasili kwa Neymar.

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Karim Benzema
Vigogo hao wa Ufaransa pia wanamtaka mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah na Robert Lewandowski wa Bayern Munich lakini Benzema anaweza kupatikana kwa urahisi kuliko wawili hao. Raia huyo wa Ufaransa anaweza kushawishika kurejea kuicheza klabu ya nyumbani.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Real Madrid watahitaji kiasi cha pauni milioni 60 au zaidi katika dili lolote litakalomhusisha Karim Benzema kwenye majira ya joto.
PSG inaweza kumsajili nyota huyu wa Real Madrid PSG inaweza kumsajili nyota huyu wa Real Madrid Reviewed by Zero Degree on 4/14/2018 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.