Loading...

Real Madrid yataja bei ya Karim Benzema

Karim Benzema
Karim Benzama ana msimu mzuri katika klabu ya Real Madrid. Mkufuzi wa klabu hiyo, Zinedine Zidane alimpa nafasi Mfaransa huyo kuonyesha thamani lakini alishindwa. Amefunga magoli 8 katika mechi 34, ikiwa ni hesabu yake mbaya ya kwanza tangu ajiunge na Madrid mwaka 2009.

Benzema amekuwa akihusishwa na kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto, huku rais wa Real Madrid, Florentino Perez akiwa na mpango wa kusajili mshambuliaji mwingine wakati dirisha la usajili litakapofunguliwa. Wamekuwa wakihusishwa na straika wa Tottenham, Harry Kane na Robert Lewandowski toka Bayern Munich.

Kwa mujibu wa Diario Gol, Real Madrid watahitaji kiasi cha pauni milioni 61 katika dili lolote la uhamisho wa Karim Benzema kwenye majira ya joto. Rais wa Klabu hiyo hataki mchezaji huyo aondoke kwa kwa dau lolote litakalokuwa chini ya hilo kwa sababu bado amesalia na muda wa kuonyesha uwezo na anaweza kuwa ongezeko lenye faida kwa timu yoyote.

Raia huyo wa Ufaransa pia anataka kwenda katika timu kubwa kwa lengo la kutaka kuthibitisha kuwa bado ni mshambuliaji mwenye hadhi ya kimataifa.

Arsenal ndio klabu pekee iliyokonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo hadi hivi sasa. Arsene wenger bado anavutiwa na nyota huyo lakini hataki kulipa pauni milioni 61 kwa ajili ya uhamisho wake. Yuko tayari kulipia kuanzia pauni milioni 35 kwa ajili ya mshambuliaji huyo.
Real Madrid yataja bei ya Karim Benzema Real Madrid yataja bei ya Karim Benzema Reviewed by Zero Degree on 4/09/2018 12:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.