Mahakama yapokea taarifa ya kitabibu kuhusu akili ya Nabii Tito
Taarifa hiyo ilipokewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi James Karayemaha ambaye ataipitia kabla ya kuamua suala hilo Aprili 13, mwaka huu. “Nimepokea taarifa ya kitabibu kuhusu Nabii Tito leo asubuhi hivyo nitaipitia ili Aprili 13, Ijumaa nitoe uamuzi,” alisema Karayemaha. Nabii Tito ambaye hakuhudhuria kesi yake mara mbili mfululizo, jana alifika mahakamani hapo baada ya Hakimu Karayemaha kutoa maagizo ya mtuhumiwa huyo kufikishwa mahakamani.
Hakimu alitoa maagizo Nabii Tito afikishwe mahakamani hapo kwa sababu amekuwa hafikishwi mahakamani kusikiliza kesi yake. Februari mwaka huu, Nabii Tito alidai ana matatizo ya akili yaliyosababisha kutaka kujiua hivyo mahakama iliamuru apimwe kujua kama kweli ana matatizo ya akili au hapana. Nabii Tito amerudishwa rumande hadi Aprili 13, mwaka huu, kesi itakapotolewa uamuzi.
Mahakama yapokea taarifa ya kitabibu kuhusu akili ya Nabii Tito
Reviewed by Zero Degree
on
4/06/2018 03:35:00 PM
Rating: