Loading...

Rais Magufuli ampa Shilingi Milioni 100, mgunduzi wa Madini ya Tanzanite


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli ameahidi kumpatia pesa kiasi cha Tsh. Milioni 100, Mgunduzi wa Madini ya Tanzanite, mzee Jumanne Ngoma imsaidie katika matibabu ya ugonjwa wake unaomsumbua wa kupooza.

Rais Magufuli ameyasema hayo leo, Aprili 6, 2018 katika eneo la Simanjiro wakati anazindua Ukuta uliojengwa kuzungushiwa Migodi ya Tanzanite, Mirerani ili kuzuia utoroshwaji wa madini hayo.

“Madini haya yalivumbuliwa na mzee Jumanne Ngoma mwaka 1967, na kupeleka sampuli kwa Geologist (mtaalam wa miamba) kwenda kuyapima, pamoja na kutambuliwa na Baba wa Taifa, Mwl Julius Kambarage Nyerere kwenye barua aliyoisani Oktoba 8, 1980 akitambua kazi nzuri ya mzee Ngoma.

“Hata alipoyavumbua hakujua yatakuwa na thamani kubwa kiasi hicho, lakini mzee Ngoma hakufaidika chochote, sasa naambiwa amepooza, nitampatia shilingi milioni 100 zikamsaidie katika matibabu,” alisema Magufuli.
Rais Magufuli ampa Shilingi Milioni 100, mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Rais Magufuli ampa Shilingi Milioni 100, mgunduzi wa Madini ya Tanzanite Reviewed by Zero Degree on 4/06/2018 04:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.