Loading...

Makonda ageukia tezi dume


Mkuu wa Mkoa wa Dar es salam Paul Makonda, anatarajia kuanza mkakati maalum wa kupima tezi dume kwa lazima nyumba kwa nyumba mkoani Dar es salaam.

Taarifa hiyo imetolewa leo na mwenyewe Paul Makonda alipokuwa akizindua warsha ya utoaji wa chanjo ya saratani ya mlango wa kizazi kwa wasichana, ikihusisha waandishi wa habari, wataalamu wa afya, viongozi mbalimbali wa dini na siasa, na kusema wakati saratani ya mlango wa kizazi ikiwaathiri wanawake nchini, tezi dume inaumiza zaidi akina baba, lakini hakuna mwamko wa kulizungumzia jambo hilo.

“Kuna kasumba kuwa saratani ya tezi dume inapimwa kwa kidole jamani siyo kweli, kuna kipimo cha damu na ni rahisi hivyo nina mkakati wa kupita nyumba kwa nyumba katika mkoa wangu, kuhakikisha hii kasi ya vifo vya kina baba kwa tatizo la tezi dume inapungua kwa kuwagundua mapema na kuwaanzishia matibabu”, amesema Paul Makonda.

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa huyo wa Dar es salaam amewataka viongozi wote wa serikali za mitaa na viongozi wa dini kutoa elimu kwa jamii ili wasichana wote wafike kwenye vituo vya afya vinavyotoa chanjo hiyo kwa wingi kupata chanjo.
Makonda ageukia tezi dume Makonda ageukia tezi dume Reviewed by Zero Degree on 4/22/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.