Loading...

Barcelona wanataka kumsajili nyota huyu wa EPL kwa kubadilishana na Dembele


Ousmane Dembele alijiunga na Barcelona akitokea Borussia Dortmund kwenye majira ya joto mwaka jana, baada ya kuonyesha kiwango cha kuvutia nchini Ujerumani. Lakini ameshindwa kuishi maisha aliyoyategemea na hajawa na uhakika wa namba katika klabu yake mpya.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 21 amekuwa na wakati mgumu zaidi baada ya kuwasili kwa Philippe Coutino akitokea Liverpool mwezi Januari na Antoine Grizmann akihusishwa na vigogo hao, uwezekano wa yeye kusalia kwenye kikosi cha Barcelona unaweza kuwa mdogo sana.

Kwa mujibu wa taarifa ya Diario Gol, Barcelona wanapanga kumjumuisha Ousmane Dembele kwenye dili ambalo wanaamini Mohamed Salah atashawishika kuondoka Anfield kwenda Camp Nou.

Ripoti hiyo inaeleza kwamba, pendekezo hilo linampendeza Lionel Messi, ambaye asingependelea kumuona Antoine Griezmann akijiunga na Barcelona kwa sababua anahisi mara nyingi watakuwa na mwingiliano uwanjani.

Mohamed Salah
Salah ni miongoni mwa wachezaji wanaovutia msimu huu. Amekuwa mchezaji bora kwa Liverpool katika msimu wake wa kwanza, akifunga magoli 41 kwenye michuano yote na kuisaidia timu yake kufika hatua ya nusus fainali ya Ligi ya Mabingwa.

Kama raia huyo wa Misri atatua Nou Camp, itakuwa na maana kwamba Barcelona ina mchezaji ambaye yuko kwenye ngazi za juu badala ya kusubiri kuimarika kwa kiwango cha Dembele kuendana na matakwa yao, na pia itamaanisha Coutinho atakazania zaidi kuchukua nafasi ya Andres Iniesta katika kiungo badala ya kucheza kama winga.
Barcelona wanataka kumsajili nyota huyu wa EPL kwa kubadilishana na Dembele Barcelona wanataka kumsajili nyota huyu wa EPL kwa kubadilishana na Dembele Reviewed by Zero Degree on 4/22/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.