Loading...

Man United ina mpango wa kufanya usajili mkubwa unaomjumuisha Pogba

Paul Pogba
Manchester United ilimsajili Pogba kutoka Juventus karibu miaka miwili iliyopita, Mfaransa huyo akijikuta kwenye wakati mgumu tangu awasili Old Trafford.

Kiungo huyo wa timu ya taifa ya Ufaransa alisimama kama mchezaji tegemezi wakati Manchester United ikiibuka na ushindi dhidi ya Manchester City wiki iliyopita, akifunga magoli mawili kipindi cha pili.

Mwaka 2016, kiungo huyo alikuwa gumzo barani Ulaya. Akiwa ameushangaza ulimwengu kwa kiwango chake alipokuwa Juventus, saini yake iligombewa na klabu kadhaa zikiwemo Real Madrid na Barcelona.

Neymar Jr
Ripoti za nchini Ufaransa zinadai kwamba Paul Pogba anaweza kupwelekwa PSG kama sehemu ya ofa ya Manchester United kumnasa nyota wa timu ya taifa ya Brazil na klabu hiyo, Neymar.

Neymar alijiunga na Paris Saint-Germain kwenye majira ya joto mwaka jana kwa ada ya uhamisho iliyovunja rekodi ya Dunia.
Man United ina mpango wa kufanya usajili mkubwa unaomjumuisha Pogba Man United ina mpango wa kufanya usajili mkubwa unaomjumuisha Pogba Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 08:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.