Loading...

Rais asaini Sheria ya Pedi bure kwa Wanafunzi


RAIS wa Kenya, Uhuru Kenyatta amesaini muswada wa sheria mpya ambayo sasa itakuwa sheria kamili, inayoitaka serikali kugawa pedi bure kwa wanafunzi wote wa kike nchini humo.

Kenyatta amesaini sheria hiyo jana Jumanne, Aprili 10, ambayo pia inaitaka serikali kuweka mazingira salama kwa wanafunzi hao kuweza kuhifadhi pedi zao.

“Sheria ya Marekebisho ya Elimu ya Msingi, kuweka wajibu wa kutoa taulo za usafi (pedi) za kutosha na za ubora kwa kila mtoto msichana aliyesajiliwa na kujiandikisha katika taasisi ya elimu ya msingi ya umma na kufikia ujira, kwa serikali”, imesema taarifa ya serikali ya Kenya.

Aidha, Ripoti ya UNESCO ya mwaka 2016 imeeleza kwamba binti mmoja kati ya 10 kwenye nchi zilizopo kusini mwa jangwa la Sahara, anakosekana shuleni kwa siku ambazo yupo kwenye hedhi, kutokana na kukosa pedi za kujistiri.
Rais asaini Sheria ya Pedi bure kwa Wanafunzi Rais asaini Sheria ya Pedi bure kwa Wanafunzi Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 08:21:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.