Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 11 Aprili, 2018

Meneja wa Liverpool, Jurgen Klopp
'Manchester City ni timu bora duniani lakini nilitambua kuwa tuna uwezo wa kuwafunga.' - Klopp. (talkSport)

Mkurugenzi Mkuu wa Juventus, Giuseppe Marotta anasema anataka kiungo wa Liverpool na timu ya taifa ya Ujerumani, Emre Can kuamua ikiwa anataka kujiunga na klabu hiyo au la ndani ya siku 10. (Tuttosport)

Mshambuliaji wa Real Madrid na timu ya taifa ya Wales, Gareth Bale haondoki Real Madrid msimu huu, licha ya kupigwa benchi katika kadhaa. (ESPN)

Meneja wa klabu ya Chelsea, Antonio Conte anapigiwa upatu kuchukua nafasi ya meneja wa Paris Saint-Germain, Unai Emery. (Guardian)

Beki wa zamani wa klabu ya AC Milan anataka kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Italia.

Aliyekuwa kiungo wa klabu ya Tottenham, Ryan Mason ameanza safari ya kazi ya ukocha rasmi.

Mshambuliaji wa klabu ya Arsenal, Forward Reiss Nelson, mwenye umri wa miaka 18, anatarajia kusaini mkataba the Gunners mara baada ya kucheza mchezo wake wa kwanza katika Ligi kuu ya Uingereza dhidi ya Southampton Jumapili.

Manchester United, Chelsea na Everton zinawania saini ya mshambuliaji wa klabu ya Watford, Richarlison.

Ben Wilmot
Klabu ya Watford imejitoa kwenye mbio za kuwania saini ya beki wa Stevenage, Ben Wilmot.

Joe Hart anaamini kwamba, West Ham imekuwa timu hatari sana katika Ligi Kuu ya Uingereza kwa sasa.

Uzoefu wa mashabiki kwenye Ligi ya Mabingwa umeisaidia klabu ya Liverpool kutinga nusu fainali ya michuano hiyo, kwa mujibu wa Craig Bellamy.

Aliyekuwa meneja wa West Brom, Alan Pardew atazungumza kwa niaba ya mshambuliaji wa klabu hiyo, Jay Rodriguez katika tume huru.

Bryan Klug ameteuliwa kuwa meneja wa muda wa klabu ya Ipswich kufuatia kuondoka kwa Mick McCarthy. (Sky Sports)

Anthony Martial anataka kuhakikishiwa nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United baada ya kuwa na wakati mugumu chini ya Jose Mourinho.

Chipukizi wa klabu ya Chelsea, Martell Taylor-Crossdale anawindwa na klabu ya Fleetwood Town pamoja na Charlton Athletic. (Daily Mail)

Atletico Madrid wako tayari kumpa Antoine Griezmann ofa kubwa ya mkataba mpya katika jaribio la kumshawishi asiondoke kwenye majira ya joto.

Henrikh Mkhitaryan
Henrikh Mkhitaryan atakosa sehemu yote ya msimu iliyobaki - isipokuwa kama  Arsenal itafika fainali ya Ligi ya Europa.

Meneja wa West Ham, David Moyes anapanga kumsajili aliyekuwa kiungo wa Manchester United, Shinji Kagawa kwa pauni milioni 12.

Juventus inamfuatilia Mousa Dembele baada ya nyota huyo kukataa kusaini mkataba mpya katika klabu ya Tottenham.

Liverpool, Tottenham na klabu nyingine tatu kutoka Ligi Kuu ya Uingereza ziko kwenye ushindani mkubwa kuwania saini ya nyota wa klabu ya Norwich, James Maddison na Josh Murphy.

Sam Allardyce amemwambia Wayne Rooney kwamba umaarufu wake sio kigezo cha kupewa nafasi anayotaka katika dimba la Goodison. (Mirror)

Juventus wanajaribu kumnasa straika wa klabu ya Manchester United, Anthony Martial, huku kukiwa na uvumi unaomhusisha Mfaransa huyo na kuondoka Old Traford. (Telegraph)

Alvaro Morata anaweza kuondoka katika klabu ya Chelsea na kurejea Juventus.

Ryan Bertrand anatarajiwa kuondoka Southampton kwenye majira ya joto - hata kama klabu hiyo haitashuka daraja. (Sun)

Anthony Martial
Juventus itakabiliana na PSG kuwania saini ya mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 11 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 11 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 11:10:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.