Loading...

Watu 247 wafa kwenye ajali ya ndege


Watu wapatao 247 waliokuwa wakisafiri kwa ndege ya jeshi wamefariki dunia baada ya ndege hiyo kuanguka karibu na kambi ya jeshi ya Boufarik nje kidogo ya jiji la Algiers, vyombo vya habari vimeripoti.

Ripoti za vyombo vya habari zinasema ndege hiyo aina ya Ilyushin Il-76, ilikuwa imewabeba askari kadhaa.

Mtandao wa Algerie24, umeripoti kwamba ndege hiyo ilikuwa inaelekea katika mji wa Magharibi wa Bechar.

Picha zilizowekwa kwenye mtandao huo zimeonyesha moshi mzito ukifuka kutoka eneo ambalo ndege hiyo imeangukia huku watu wakikimbilia kutoa msaada.

Tukio la ndege hiyo kuanguka Boufarik ndiyo baya zaidi kwa Algeria tangu mwaka 2003 wakati ndege ya Shirika la Air Algerie ilipoanguka muda mfupi baada ya kuruka kutoka uwanja wa Tamanrasset na iliua watu 102.

Mwaka 2014, zaidi ya wanajeshi 70 pamoja na familia zao walikufa pale ndege ya C-130 ilipoanguka kwenye milima ya Djebel Fertas muda mfupi kabla ya kutua kwenye mji wa Kaskazini wa Constantine.

Desemba 2012, ndege mbili za kijeshi zilizokuwa zinafanya mazoezi ya kawaida ziligongana angani karibu na mji wa Tlemcen ulioko Kaskazini Magharibi na kuua marubani wa ndege zote mbili.
Watu 247 wafa kwenye ajali ya ndege Watu 247 wafa kwenye ajali ya ndege Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 12:25:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.