Loading...

Je, Droo ya nusu fainali ya UEFA ni lini? Nani atapangwa na Liverpool au Roma?


Ligi ya Mabingwa inarejea wiki hii, ikiwa ni mzunguko wa pili wa mechi za robo fainali za msimu huu zinazochezwa Jumanne na Jumatano.

Hapa chini kuna maelezo yote ambayo unatakiwa kujua kuelekea droo ya nusu fainali ya michuano hii.

Real Madrid iko mbele ya Juventus, ikiwa imeshinda goli 3-0 ugenini wiki iliyopita, wakati Bayern Munich ikifanikiwa kuondoka na magoli mawili ya ugenini katika ushindi wao wa goli 2-1 dhidi ya Sevilla.

Liverpool tayari wamefuzu kwa hatua ya nusu fanali kwa kuitoma Manchester City kwa jumla ya magoli 5-1 siku ya Jumanne usiku, wakati Roma ikiiduwaza Barcelona na kutinga nusu fainali kwa faida ya goli la ugenini.

Mechi nyingine za mzunguko wa pili wa robo fainali zitachezwa leo, Bayern itacheza dhidi ya Sevilla wakati Real Madrid ikiikaribisha Juventus saa 3:45 usiku.
Droo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa itafanyika saa 7:00 mchana Ijumaa ya tarehe 13 Aprili Nyon, Uswisi. Hakutakua na kizuizi chochote, hivyo yeyote anaweza kupangwa na timu yoyote.

Mechi za mzunguko wa kwanza wa nusu fainali zitachezwa Jumanne ya tarehe 24 April na Jumatano ya tarehe 25 April kisha mechi nyingine za mzunguko wa pili wa nusu fainali zitachezwa wiki moja baadaye.

Yeyote atakayekuwa wa kwanza kuchaguliwa katika drooo hiyo ataanzia mechi yake ya mzunguko wa kwanza nyumbani.

Fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa 2018 itachezwa Jumamosi ya Mei 26 saa 3:45 usiku, kwenye uwanja wa Olympic Stadium mjini Kiev, Ukraine.
Je, Droo ya nusu fainali ya UEFA ni lini? Nani atapangwa na Liverpool au Roma? Je, Droo ya nusu fainali ya UEFA ni lini? Nani atapangwa na Liverpool au Roma? Reviewed by Zero Degree on 4/11/2018 12:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.