Loading...

Mbeya City, Yanga zagawana pointi


Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania bara Yanga, wamebanwa mbavu ugenini na Mbeya City na kutoka sare ya bao 1-1 kwenye mchezo uliomalizika jioni hii kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya.

Mchezo huo ambao uligubikwa na vurugu za hapa na pale ulishuhudia wageni Yanga, wakifunga bao la kuongoza dakika ya 57 kupitia kwa kiungo Raphael Daud ambaye amesajiliwa msimu huu kutoka Mbeya City.

Bao hilo lilisababisha vurugu za mashabiki lakini baadae walitulia na mchezo ukaendelea hadi dakika ya 67 ambapo mlinzi wa kati wa Mbeya City Ramadhan Malima kuoneshwa kadi nyekundu baada ya kumchezea rafu Juma Abdul.

Mashabiki walianza kurusha mawe uwanjani na kupelekea Jeshi la polisi kutumia mabomu ya machozi kuweza kutuliza vurugu hizo na mchezo kuendelea. Mbeya City waliendelea kucheza pungufu.

Tukio la mvuto zaidi katika mchezo wa leo ni bao la kusawazisha la Mbeya City ambalo limefungwa dakika ya 90 na mshambuliaji ambaye aliingia akitokea benchi na kufunga bao hilo ambalo limeamua mchezo umalizike kwa sare.
Mbeya City, Yanga zagawana pointi Mbeya City, Yanga zagawana pointi Reviewed by Zero Degree on 4/22/2018 06:15:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.