Loading...

Mbunge aishauri serikali kufuta upinzani


Mbunge wa Viti Maalum wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecilia Pareso amefunguka na kuishauri serikali ya awamu ya tano kama inataka ivifute kabisaa vyama vya upinzani nchini kwa sababu inaonyesha haivitaki vyama hivyo.

Cecilia Pareso amesema hayo bungeni jana na kusema kuwa serikali imekuwa ikitumia nguvu kubwa na jitihada kubwa kuuwa vyama vya upinzani nchini kwa kuvinyima haki yake ya msingi ikiwa pamoja na kueneza sera zake kwa wananchi pamoja na viongozi mbalimbali wa vyama hivyo kukamatwa na kufungwa kwa matakwa vya serikali.

"Maana tuliingia kwenye uchaguzi kati ya vyama vya upinzani na jeshi la polisi, hivyo ushauri wangu kwa sababu inaonekana mmeongeza adui mwingine ambaye hamtaki kumsikia wala hamtaki kuona vyama vya upinzani vikifanya kazi yao. Ushauri wangu Waziri Mkuu kwa serikali yako ni kuleta marekebisho ya Katiba hapa bungeni tufute vyama vingi ulimwengu ujue, dunia ijue kwamba serikali ya awamu ya tano haitaki kabisa mfumo wa vyama vingi turudi kwenye mfumo wa chama kimoja. Mimi nadhani hiyo ndiyo njia bora na mtaendelea kufanya unayoyafanya kadili mnavyotaka" alisisitiza Pareso
Mbunge aishauri serikali kufuta upinzani Mbunge aishauri serikali kufuta upinzani Reviewed by Zero Degree on 4/06/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.