Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 6 Aprili, 2018

Luke Shaw
Barcelona wanatazamia kumsajili beki wa Manchester United, Luke Shaw kwa mkopo.

Leicester inakabiliana na Crystal Palace pamoja na Swansea kwenye mbio za kuwania saini ya winga wa klabu ya Celta Vigo, Daniel Wass. (Sun)

Barcelona imetozwa faini na UEFA kufuatia kitebdo cha utovu wa nidhamu kilichojitokeza kwenye mchezo wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Roma.

Golikipa wa Bayer Munich, Manuel Neuer amerejea kwenye mazoezi ya klabu hiyo baada ya miezi 6.

Fabinho amesema kuwa hajafanya mawasiliano yoyote na klabu ya PSG juu ya uhamisho wake. (ESPN)
  
Gatuso amepewa mkataba mpya katika klabu ya AC Milan kufuatia mafanikio yaliyopatikana tangu achukue madaraka ya kuinoa klabu hiyo. (SkySports)

Galatasary wameonyesha nia ya kumsajili aliyekuwa kiungo wa Manchester United, Shinji Kagawa. (Bild)

Christian Koffi
Liverpool wanapewa nafasi kubwa ya kufanikisha usajili wa chipukizi wa klabu ya Monaco, Christian Koffi, ambaye mkataba wake unaisha kwenye majira ya joto.

Mkufunzi wa Montreal Impact ana nia ya kumsajili Hatem Ben Arfa wakati mkataba wake na PSG utakapoisha kwenye majira ya joto. (L'Equipe)

Mshambuliaji wa Liverpool, Mohamed Salah ana uhakika atakuwa fit kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Everton Jumamosi.

Thomas Tuchel 'atakuwa' meneja mpya wa Paris Saint-Germain kwenye majira ya joto, kwa mujibu wa ripoti. (Daily Mail)

Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes anafanya mipango ya usajili wa msimu ujao, akiwa na mpango wa kujaribu kumnasa kiungo wa klabu ya Norwich, James Maddison, wa Bournemouth, Harry Arter na Ryan Fredericks kutoka Fulham. (Express)

Golikipa Martin Dubravka ana matumaini ya kuendelea kuitumikia Newcastle hadi baada ya mkataba wake wa mkopo kutoka Sparta Prague utakapoisha.

Emre Can
Emre Can anaweza kuukosa mchezo wa Liverpool dhidi ya Everton Jumamosi na vile vile anaweza kulikosa Kombe la Dunia kutokana na majeraha ya mgongo.

Roy Hodgson anaweza kumchagua Christian Benteke licha ya kuwa straika huyo kutoka kwenye majeruhi hivi karibuni.

Meneja wa Swansea, Carlos Carvalhal amekataa kusaini mkata mpya wa zaidi ya mwaka mmoja katika klabu hiyo. (Mirror)

Liverpool watasafiri kwenye Manchester katika siku ya mchezo wao wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Man City.

Mshambuliaji wa Stoke City, Saido Berahino ameondolewa kwenye kikosi cha kwanza baada ya kuchelewa kwenye mechi ya timu hiyo ya wachezaji chini wenye umri chini ya 23, siku ya Jumatatu. (Telegraph)

Nyota wa klabu ya Liverpool, Alex Oxlade-Chamberlain amewasifu mashabiki wa timu hiyo kwa kutengeneza mazingira ya ushindi katika mchezo wao dhidi ya Man City. (Guardian)

Leigh Griffiths anatazamia kusaini mkataba mwingine na klabu ya Celtic ambao utamfanya aitumikie klabu hiyo hadi mwisho wa maisha yake ya soka.

Craig Levein anasema kuwa ,azungumzo ya mkataba mpya na Harry Cochrane, mmoja kati ya wachezaji tegemezi wa klabu ya Hearts yanaendelea. (Record)

Sokratis Papastathopoulos
Man United ina mpango wa kumsajili beki wa Borussia Dortmund, Sokratis Papastathopoulos, ambaye mkataba wake unaisha mwaka 2019. (Kicker)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 6 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 6 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/06/2018 10:36:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.