Loading...

Rais Jacob Zuma afika Mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili


Kesi ya rushwa ya aliyekuwa Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ya anayekabiliwa na tuhuma 16 zikiwemo za udanganyifu, ufisadi na kutakatisha fedha haramu wakati akiwa madarakani, imehairishwa hadi Juni 8, 2018, itakaposomwa tena.

Zuma alifika Mahakama Kuu ya Durban leo asubuhi Aprili 6, 2018 kwa ajili ya kusikiliza kesi yake hiyo ambayo huku wafuasi wake walijikusanya maeneo ya karibu ya mahakama hiyo huku wakiimba nyimbo za kumsifu, wakisema hawatamuacha mpaka mwisho, na wengine wakikikesha kumuombea.

Zuma alifunguliwa mashtaka na kesi yake kusikilizwa kisha kufutwa mwaka 2009 na sasa imeanza kusikilizwa tena baada ya kuondolewa madarakani na kumuachia Cyril Ramaphosa ambaye aliahidi kukomesha vitendo vya rushwa na ufisadi nchini humo.
Rais Jacob Zuma afika Mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili Rais Jacob Zuma afika Mahakamani kujibu mashtaka yanayomkabili Reviewed by Zero Degree on 4/06/2018 04:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.