Serikali kujenga makumbusho ya Marais Wastaafu
Hayo yameelezwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla wakati akizungumza na Balozi wa Uingereza hapa nchini, Sarah Cooke ofisini kwake mjini Dodoma.
Dk. Kigwangalla amemueleza balozi Cooke kuwa, Serikali kupitia Wizara yake inaendelea kuimarisha vivutio vya utalii hapa nchini kwa kupanua jeografia ya maeneo ya utalii sambamba na kuongeza vivutio ili kuongeza idadi ya watalii na mapato.
Amesema Serikali itajenga makumbusho ya Marais Wastaafu wa Tanzania mjini Dodoma pamoja kuanzisha makumbusho ya meno ya tembo katika miji ya Dar es Salaam, Arusha, Iringa na Dodoma.
Sambamba na hayo amesema Serikali itaanzisha mwezi maalum wa maadhimisho ya urithi wa Mtanzania ambao utafanyika mwezi Septemba kila mwaka pamoja na kuendeleza utalii wa mikutano.
Amesema Serikali pia itaanzisha Mamlaka ya Usimamizi na Uendelezaji wa Fukwe nchini ili kuimarisha utalii wa fukwe pamoja na kutambua barabara iliyokuwa ikitumika katika biashara ya utumwa wakati wa ukoloni ili iweze kutumika kiutalii.

Reviewed by Zero Degree
on
4/19/2018 12:18:00 PM
Rating: