Waziri Mkuu awaonya wabunge
Waziri Majaliwa ametoa kauli hiyo leo Aprili 19, 2018 Bungeni jijini Dodoma kwenye kikao cha 13 mkutano wa 11 wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati akijibu swali la Mbunge Abdalla Mtolea ambapo alitaka kujua serikali ina mpango gani wa kuhakikisha madhara yanayojitokeza katika jiji la Dar es Salaam na mvua kudhibitiwa?
Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema..
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa pole wananchi wote walioweza kupata maafa ya aina yeyote yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini
"kupitia Manispaa za jiji la Dar es Salaam na serikali yake kupitia wizara zake zinazo mipango ya kuboresha miundombinu katika miji yetu katika makao makuu ya mikoa na maeneo yote yale yanayokaliwa na watu wengi ikiwepo DSM. Tunayo miradi sasa ambayo itaweza kuboresha miundombinu ikiwepo na bonde la Msimbazi ambalo linaleta madhara mengi...
Mara kadhaa tumeshuhudia mvua hizi zinapoleta madhara kwa wale walioko mabondeni pamoja na serikali kuwaambia waondoke mabondeni tumekuwa tukiingilia sana utendaji kwa kuingiza siasa za kuwataka watu wabaki huku wengine wakijafanya wanawaonea huruma na kushindwa kutoka katika mabonde kutokana na utetezi unaotoka kwa watu wenye mapenzi yao binafsi", amesema Majaliwa.
Waziri Mkuu ameendelea kwa kusema..
"Nitoe wito kama ambavyo tunaendelea kutoa wito na Waheshimiwa Wabunge kupitia Bunge hili tuwasii watanzania na kuwataka wote wanaoishi mabondeni wahame kwasababu mvua hizi zinapokuja wanapata madhara makubwa na hatimaye sasa hata katika kuwaokoa inakuwa shida. Kwa hiyo ni vizuri sasa tukashirikiana".
Pamoja na hayo, Majaliwa ameendelea kwa kusema "serikali kwa upande wake inaanda fedha kuhakikisha kwamba ile miundombinu ya mabonde ina boreshwa ili maji yaweze kupita kwa ulaini. Lakini watu waliokaa katika mabonde na yale maeneo yote waliyokataziwa waanze kuondoka mapema ili wasiweze kupata madhara pindi mvua nyingi zinapojitokeza".
Kwa upande mwingine, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewapa pole wananchi wote walioweza kupata maafa ya aina yeyote yaliyosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha nchini
Waziri Mkuu awaonya wabunge
Reviewed by Zero Degree
on
4/19/2018 12:35:00 PM
Rating: