Loading...

Serikali yakanusha kuhusu hoja ya Nape


Serikali ya awamu ya tano iliyopo chini ya Rais Magufuli imefunguka na kukanusha taarifa za kutelekeza mradi wa gesi asili kwenye kuzalisha umeme kama alivyodai Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye wakati alipokuwa anatoa maoni yake juu ya hotuba ya Waziri Mkuu Kasim Majaliwa Bungeni.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani leo (Aprili 10, 2018) kwenye mkutano wa 11 kikao cha sita kinachoendelea kufanyika mkoani Dodoma pindi alipokuwa anatoa maelezo ya jumla kwa baadhi ya hoja zilizotolewa na Wabunge katika kikao cha Bunge cha 11 zilizoelekezwa katika Wizara yake hususan suala la vyanzo vya kuzalisha umeme kwa upande wa gesi asilia pamoja na maji ambalo lilitajwa kwa kiasi kikubwa na Mbunge Nape aliyedai serikali imewasaliti wananchi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara kutokana na kutoonekana neno gesi kwenye hotuba ya Waziri Mkuu yote.

"Nianze kuwatoa wasiwasi wabunge, kwamba sio kweli kuwa vyanzo vya maji vinavyotumika kuzalisha umeme havijatajwa katika Ilani ya uchaguzi wa CCM ya mwaka 2015 kama ilivyokuwa imedaiwa hapo awali. Ilani imetaja vyanzo haijabainisha mradi kwa mradi. Katika Ilani yetu ya CCM aya 43.a imeeleza vyanzo vya msingi ambavyo serikali itavielekeza katika kuzalisha umeme wa uhakika na unaotabirika kwa gharama nafuu na vyanzo vya maji vikiwemo", amesema Dkt. Kalemani.

Pamoja na hayo, Dkt. Kalemani ameendelea kwa kusema "ukienda kwenye mpango wa miaka wa miaka 5, ukurasa wa 81 umetaja bayana kadharika, vyanzo halali vitakavyotupungukia bugudha, tofauti ndogo ndogo na migogoro ya upungufu ya umeme ikiwemo vyanzo vya gesi ya asilia, maji, makaa ya mawe pamoja na upepo. Tunapotaja vyanzo vya kuzalisha umeme kimsingi hatutaji mradi kwa mradi".

Dkt. Kelemani amesisitiza kuwa...

"Serikali haitaweza kutelekeza kutumia gesi ya asilia hivi sasa tunayo Tilioni 57.5 ya gesi asilia na umeme kwa kiasi kikubwa tunaotumia sasa hivi zaidi ya MW 787 zinatokana na gesi asilia. Kwa hiyo sio kweli kwamba tumetelekeza matumuzi ya gesi asilia".

Kwa upande mwingine, Dkt. Kalemani amesema bado matumizi ya gesi ya asili ni makubwa na serikali wapo makini nalo kwa hilo sana.
Serikali yakanusha kuhusu hoja ya Nape Serikali yakanusha kuhusu hoja ya Nape Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 12:16:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.