Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Aprili, 2018

Yaya Toure
Kiungo wa Manchester City na timu ya taifa ya Ivory Coast, Yaya Toure, ambaye mkataba wake Etihad unaisha kwenye majira ya joto anaweza kujiunga na klabu ya Fernabache.

Nyota wa RB Lepizig, Dayot Upamecano amesema kuwa ana ndoto na kuichezea Real Madrid, Barcelona au Manchester United.
 
Gareth Bale anaipenda sana klabu ya Real Madrid na hakuna ukweli wowote juu ya taarifa ambazo zinazungumzia uhamisho wake, kwa mujibu wa wakala wa mshambuliaji huyo wa timu ya taifa ya Wales. (ESPN)

Meneja wa Everton, Sam Allardyce anatazamia kumsajili beki wa klabu ya West Ham, Aaron Cresswell anayekadiriwa kuwa na thamani ya karibu pauni milioni 25. (talkSport

Isco anatarajiwa kuondoka Real Madrid kwenye majira ya joto lakini hadi hivi sasa bado haijafahamika atajiunga na klabu ipi. (Don Balon)

Jina la Thomas Tuchel limetawala kwenye vichwa vya habari vya magazeti ya Ufaransa, huku Mjerumani huyo akitarajiwa kutua PSG msimu ujao. 
 
Paris Saint-Germain na Monaco zitakabiliana kuwania saini ya Marouane Fellain, ambaye atakuwa mchezaji huru kwenye majira ya joto. (L'Equipe)

Mshambuliaji wa Manchester United, Antony Martial amehusishwa tena na uhamisho kwenda Juventus.

Jina la mshambuliaji wa Juventus, Mario Mandzukic linaweza kuwa jina pili kubwa kwenda Ligi Kuu ya China kutoka barani Ulaya. (Tuttosport)

Sam Johnstone
Sam Johstone, ambaye anaichezea Aston Villa kwa mkopo akitokea Manchester United amesema kuwa hawezi kuendelea kuwa mchezaji wa Manchester United hadi mwisho.
 
Kiungo wa Arsenal, Reiss Nelson ana matumaini ya kusaini mkataba mpya ndani ya wiki kadhaa zijazo.

Bayern Munich na PSG ziko tayari kumsajili winga wa klabu ya Chelsea, Kenedy kama atawekwa sokoni. Raia huyo wa Brazil kwa sasa anayeichezea Newcastle kwa mkopo.

Aliyekuwa nyota wa timu ya taifa ya Scotland, Scott Booth anatarajia kuona meneja wa klabu ya Aberdeen anasalia na kuendeleza mapambano katika klabu hiyo inayoshirirki Ligi Kuu ya Scotland. (Sky Sports)

Marcus Rashford anaendelea kuumizwa na kitendo cha kukosa muda wa kutosha kwenye kikosi cha kwanza cha Manchester United.

Tottenham wanatarajia kuingia kwenye orodha ya timu 10 kwa utajiri barani Ulaya wakati watakapohamia kwenye Uwanja wao mpya 'White Hart Lane' msimu ujao.

Andy Carroll yuko fit kwa ajili ya kuitumikia West Ham katika michezo sita iliyosalia msimu huu.

West Brom wanatarajia kupoteza wachezaji wengi kwenye majira ya joto, huku Salomon Rondon akitajwa kuwa mchezaji anayeweza kuondoka mapema baada ya msimu msimu huu kumalizika. (Mirror)

Ben Wilmot
Watford imezipiku Arsenal na Spurs kwenye mbio za kuwania saini ya chipukizi kutoka Uingereza, Ben Wilmot anayeichezea klabu ya Stevenage.

Pep Guardiola ameapa kwamba hakutakuwa na suala la kulipa kisasi kwa kile alichofanyiwa na mashabiki wa Liverpool katika dimba la Anfield wiki iliyopita.

Pep Guardiola amepata pigo kubwa kufuatia mechi ya Manchester City dhidi ya Liverpool kwenye Ligi ya Mabingwa kupangiwa mwamuzi ambaye hivi karibuni alikosolewa na Mhispania huyo.

Joe Hart bado ana mapenzi na mchezo wa mpira wa miguu licha ya kuwa na wakati mgumu katika klabu ya West Ham. (Sun)
Gareth Bale amedhihakiwa kwa ada yake ya uhamisho na aliyekuwa meneja wa Real Madrid, Jorge Valdano. (Express)

Salomon Rondon anaweza kuondoka West Brom kwa pauni milioni 16.5 kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Chelsea hawana mpango wa kuvunja mkataba wa Antonio Conte kabla msimu haujaisha licha ya kuwa na mwisho mbaya na kubaki wakitegemea michuano ya FA Cup pekee. (Times)

Kampuni ya Adidas iko kwenye mazungumzo ya kina na klabu ya Arsenal juu ya dili lenye thamani ya pauni milioni 40 kwa msimu.

Javier Hernandez
Javier Hernandez amemwambia meneja wa West Ham, David Moyes kuwa hafurahii kitendo cha kuanzia benchi. (Daily Mail)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 10 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/10/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.