Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 26 Aprili, 2018

Marouane Fellaini
Marouane Fellaini anatafakari juu ya kuondoka Manchester United baada ya Roma, Marseille na klabu za China kuonyesha nia ya kumsajili.

Andres Iniesta alistahiri kupewa tuzo ya Ballon d'Or, kwa mujibu wa beki wa klabu ya Real Madrid, Sergio Ramos. (ESPN)
  
Aliyekuwa beki wa klabu ya Tottenham, Yuri Berchiche anaweza kurejea nchini Uhispania kwenye majira ya joto. (Le10Sport)

Golikipa wa Bayer Leverkusen, Bernd Leno anaweza kuondoka kwenye majira ya joto. (Kicker)

Real Madrid haijafanya mawasiliano yoyote na Liverpool juu ya uhamisho wa Mohamed Salah.

Christian Benteke anakiri kuwa kushuka kwa kiwango chake kunaweza kumkosesha nafasi katika timu yake ya taifa kwenye Kombe la Dunia.

Pablo Hernandez amesaini mkataba mpya na klabu ya Leeds utakaomfanya aendelee kuitumikia klabu hiyo hadi kwenye majira ya joto mwaka 2020.

Aliyekuwa meneja wa klabu ya Manchester United, Louis van Gaal amesema kuwa amepewa ofa ya kurejea kwenye kazi hiyo ya ukufunzi ambayo hawezi kuikataa.

Zlatan Ibrahimovic
Shirikisho la Soka la Uswidi limetangaza kuwa mshambuliaji wao, Zlatan Ibrahimovic hatacheza Kombe la Dunia mwaka huu. (Sky Sports)

Arsene Wenger anasema kuwa anataka kuwa mkufunzi wa timu nyingine kubwa barani Ulaya baada ya kuondoka Arsenal.

Chelsea wana matumaini ya kuondokana na kutumia kiasi kikubwa cha fedha kumbadilisha Antonio Conte kufuatia kuwepo kwa uhitaji wa makocha wapya katika klabu nyingi kwenye majira ya joto. (Telegraph)

Liverpool wameiambia Real Madrid kuwa pauni milioni 200 haitawasaidia kumpata Mohamed Salah.

Arsenal inakabiliana na Chelsea pamoja na Manchester United kuipata saini ya kiungo wa klabu ya Roma, Radja Nainggolan.

Leicester City wameambiwa kuwa klabu ya FC Porto inataka pauni milioni 30 kwa ajili ya beki wao wa kulia, Ricardo Pereira.

Crystal Palace ina nia ya kumsajili kiungo wa timu ya taifa ya Ubelgiji, Leander Dendoncker. (Daily Mail)

Arsene Wenger amedai kuwa ingekuwa vizuri zaidi kama Arsenal ingemleta aliyekuwa mchezaji wa zamani wa klabu hiyo achukue nafasi yake.

Jorginho
Manchester United wanatarajiwa kukabiliana na mahasimu wao, Man City kuwania saini ya kiungo wa Napoli, Jorginho.

Orodha ya Mauricio Pochettino kwenye usajili wa majira ya joto inamjumuisha winga wa Sporting Lisbon, Gelson Martins, beki wa Southampton, Cedric Soares na kiungo wa klabu ya Wolve, Ruben Neves.

Klabu ya Ipswich inaweza kumfanya Chris Coleman wa Sunderland awe meneja wao mpya kwenye majira ya joto(Mirror)

Beki wa Swansea, Alfie Mawson na Lewis Dunk wa Brighton ni vinara kwenye orodha ya wachezaji ambao meneja wa West Ham, David Moyes anawahitaji kwenye usajili wa majira ya joto. (Star)

Golikipa wa West Ham, Adrian atalazimisha kuondoka katika klabu hiyo kwenye majira ya joto kama David Moyes ataendelea kuwa meneja.

Manchester United wanataka Jonny Evans arejee katika klabu hiyo kutokea West Brom kwenye majira ya joto kwa ada pungufu ya pauni milioni 3.

Steven Gerrard yuko kwenye mazungumzo ya kuwa meneja mpya wa klabu ya Rangers.

Lucas Leiva ana mapngo wa kukaa pamoja na mashabiki wa klabu ya Liverpool wakati watakapoenda kucheza na Roma. (Sun)

Ryan Sessegnon
Manchester United wana matumaini ya kufanikiwa kumshawishi Ryan Sessegnon atue Old Traford kwenye majira ya joto kama beki huyo ataamua kuondoka Fulham kwenye majira ya joto. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 26 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Alhamisi Tarehe 26 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/26/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.