Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 20 Aprili, 2018


Arsene Wenger amethibitisha kuwa ataondoka Arsenal mwishoni mwa msimu huu na kusema kuwa aliyekuwa kiungo wa klabu hiyo, Patrick Vieira anaweza kuchukuwa nafasi yake.
Dennis Wise ameishauri Chelsea imsajili kiungo wa Arsenal, Jack Wolshere na kusistiza kwamba raia huyo wa Uingereza anaweza kuwa tegemezi kwenye kikosi cha kwanza cha timu hiyo. (Sky Sports)

Manchester United watahitaji kulipwa karibu pauni milioni 140 kwa ajili ya Paul Pogba kama ataondoka Old Trafford kwenye majira ya joto.

Arsenal watatoa ruzuku ya tiketi kwa za mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya Europa League baada ya mashabiki kulalamikia kiingilio cha pauni 79 kwa mchezo wao wa ugenini dhidi ya Atletico Madrid.

Sam Allardyce ametoa wito kwa ajili ya uwaji juu ya hatima yake katika klabu ya Everton baada ya kuaibishwa kufuatia swali aliloulizwa wakati wa utafiti wa klabu hiyo.

Shirikishi la Soka la Uingereza (FA) limefikia makubaliano na serikali pamoja na  falme ya nchi hiyo kwa kuamua kwamba hawatapeleka wafanyakazi wa ziada nchini Urusi wakati wa Kombe la Dunia. (Daily Mail)

Alexis Sanchez anaweza kuachwa nje ya kikosi cha Manchester United kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuano ya FA dhidi ya Tottenham baada ya Marcus Rashford kumshawishi Jose Mourinho kuwa anaweza kuiongoza safu ya mbele ya klabu hiyo.

Crystal Palace wako tayari kumuuza Christian Benteke kwenye majira ya joto baada ya kuchoshwa na uwezo wake mdogo mbele ya goli.

Morgan Schneiderlin
Morgan Schneiderlin ameelezea tamaa yake ya kuondoka Everton na kurejea nchini Ufaransa. (Sun)

Liverpool wanakaribia kufikia makubaliano ya dili la kandarasi ya miaka minne na nyota wa klabu ya Real Madrid, Dani Ceballos.

Arsene Wenger yuko tayari kuanza mapinduzi kwa kufanya mabadiliko ya kikosi cha Arsenal kwa kuwauza wachezaji wa klabu hiyo waliocheza chini ya kiwango akiwemo Shkodran Mustafi na Granit Xhaka.

Manchester United inaziongoza Bayern Munich na Juventus kwenye mbio za kuwania saini ya nyota wa klabu ya Watford, Richarlison.

Manchester City wanatafakari juu ya uwezekano wa kurejea sokoni kuwania saini ya Riyad Mahrez kwenye majira ya joto.

West Ham wana nia ya kumbakisha golikipa anayeichezea klabu hiyo kwa mkopo kutoka Manchester City, Joe Hart hadi msimu ujao. (Mirror)

Manchester City iko miongoni mwa vilabu vinavyowania saini ya beki chipukizi wa timu ya taifa ya Uholanzi, Matthijs de Ligt, ambapo mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo, Txiki Bergiristain alionekana Amsterdam Jumatano kwa ajili ya mkutano na masakuti wa klabu yake.

Arsene Wenger anasema kuwa anatumai ataweza kumpa Santi Cazorla ofa ya mkataba mpya katika klabu ya Arsenal lakini anakiri kuwa hajui kama kiungo huyo ataweza kucheza soka tena. (Telegraph)

Jorginho
Kiungo wa klabu ya Napoli, Jorginho ni mingoni mwa wachezaji wanaomvutia mkufunzi wa Manchester United, Jose Mourinho. (Independent)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 20 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 20 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/20/2018 11:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.