Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 16 Aprili, 2018
Ousmane Dembele |
Ousmane Dembele amekanusha taarifa zinazodai kuwa atatafuta namna ya kuondoka Barcelona kwenye majira ya joto.
Klabu ya Monaco itazingatia ofa yoyote kwa ajili ya uhamisho wa winga wa timu ya taifa ya Ufaransa, Thomas Lemar, baada ya kutolea nje ofa ya Arsenal mwezi Januari. (Telefoot)
Marco Verrati anasema kuwa anafurahia uamuzi wake wa kuchagua kubaki PSG, huku kukiwa na tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda Barcelona.
Zinedine Zidane anasema kuwa Isco ni mchezaji muhimu sana kwa klabu ya Real Madrid. (ESPN)
Arturo Vidal anaweza kuwa njiani kuondoka Bayern Munich, huku ripoti nyingi zikidai kuwa klabu hiyo ya Ujerumani itamuuza kwenye majira ya joto. (Kicker)
Manchester United inamtaka beki wa klabu ya Leicester City, Harry Miguel kwenye majira ya joto.
Meneja wa klabu ya West Ham, David Moyes amemfananisha straika wa klabu hiyo, Marko Arnautovic na aliyekuwa nyota wa Man United, Zlatan Ibrahimovic.
Mohamed Salah amesema kuwa kushinda taji la Ligi ya Mabingwa itakuwa na maana kubwa sana kwake kuliko kitu chochote msimu huu.
Alisson Becker |
Golikipa wa klabu ya Roma, Alisson Becker hatauzwa kwenye majira ya joto, kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo, James Pallota.
Manchester City itakabidhiwa rasmi taji la Ligi Kuu ya Uingereza tarehe 6 mwezi mei.
Mwenyekiti wa Paris Saint-Germain, Nasser Al-Khelaif amesema kuwa taji la Ligi ya Mabingwa linabiki kuwa lengo kuu, baada ya klabu hiyo kufanikiwa kutetea taji la Ligue 1 kwa ushindi wa goli 7-1 dhidi ya Monaco. (Sky Sports)
Roy Hodgson anasisitiza kuwa nyota anayeichezea Crystal Palace kwa mkopo kutoka Chelsea, Ruben Loftus-Cheek anastahili nafasi kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza kwenye Kombe la Dunia. (Daily Mail)
Manchester City wana matamanio makubwa ya kumnasa mshambuliaji wa klabu ya Crystal Palace, Wilfried Zaha anayekadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 50.
Golikipa wa Liverpool, Loris Karius anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.
Nyota wa Manchester City, Patrick Roberts anakiri kuwa hajui atakuwa wapi msimu ujao.
Nyota wa Leyton Orient, Macauley Bonne anazivutia klabu za Shrewsbury, Portsmouth pamoja na Bury. (Sun)
Pep Guardiola |
Pep Guardiola amewapa changamoto wachezaji wa Man City kuandika historia kama ya klabu kubwa za Uingereza.
Meneja wa klabu ya Stoke City, Paul Lambert anasema kwamba, kuiepusha klabu yake na kushuka daraja katika LIgi Kuu ya Uingerezaitakuwa moja wapo ya mafanikio yake makubwa. (Telegraph)
Rais wa klabu ya Monaco, Vadim Vasilyev amezionya Liverpool na Arsenal kwamba, Thomas Lemar atakuwa ghali zaidi kwenye majira ya joto.
Beki wa klabu ya Chelsea, Antonio Rudiger anasisitiza kwamba alikuwa fiti kuivaa Southampton na haujui ni kwanini Antonio Conte alimweka benchi.
Aliyekuwa mshambuliaji wa Chelsea, Diego Costa yuko chini ya uchunguzi kwa kukwepa kulipa kodi, kwa mujibu wa ripoti za nchini Uhispania.
Antonio Conte amewaambia wachezaji wa Chelsea kuwa wasicheze kwa lengo la kumfurahisha yeye, lakini wacheze kwa lengo la kuipa mafanikio klabu, kuipa heshima beji ya klabu na kuwafurahisha mashabiki.
Kiwango cha Joe Hart ndani na nje ya uwanja msimu huu kitakuwa kimemvutia mkufunzi wa timu ya taifa ya Uingereza, Gareth Southgate, kwa mujibu wa David Moyes. (Mirror)
Mark Hughes amewaonya wachezaji wa Southampton kwamba wanatakiwa wajitoe ili kuisaidia klabu kusalia katika Ligi Kuu ya Uingereza. (Guardian)
Sheikh Mansour |
Mmiliki wa klabu ya Manchester City, Sheikh Mansour ametuma pongezi zake kwa Pep Guardiola kwa kushinda taji la Ligi Kuu ya Uingereza. (Star)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 16 Aprili, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
4/16/2018 11:35:00 AM
Rating: