Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Aprili, 2018

Javier Pastore
Chelsea na Liverpool zitarejea sokoni kuwania saini ya kiungo mshambuliaji wa klabu ya PSG, Javier Pastore kwenye majira ya joto.

Manchester United haitamzuia Luke Shaw kuondoka lakini klabu itakayomtaka italazimika kulipia kiasi cha pauni milioni 28 kwa ajili ya beki huyo wa timu ya taifa ya Uingereza.

Tottenham itawania saini ya golikipa wa Manchester United, Sam Johnstone kwenye majira ya joto. (talkSport)

Juventus inatazamia kufanya mabadiliko makubwa kwenye majira ya joto na inakaribia kuanza mchakato wa kumsajili Matteo Darmian na Emre Can.

Mauricio Pochettino atatafakari juu ya kuacha kuipa uzito michuano ya FA Cup ya msimu ujao kwa kuwapa nafasi wachezaji chipukizi wa Tottenham kwenye michuano hiyo. (Daily Mail)

Neymar inambidi aondoke Paris Saint-Germain, kwa mujibu wa aliyekuwa nyota klabu ya Barcelona na timu ya taifa ya Brazil, Rivaldo.

Borussia Dortmund inamvizia chipukizi wa klabu ya Gremio, Victor Bobsin anayecheza nafasi ya kiungo mkabaji. (ESPN)
 
Jose Mourinho anasema kuwa mashabiki watakuwa tayari ''kumuua'' kama Manchester United haitashinda taji la michuano ya FA.
 
Paul Pogba
Paul Pogba amesistiza kuwa lengo lake kubwa ni kuitumikia Manchester United kwa nguvu zake zote wala hafikirii juu ya uhamisho wake, huku kukiwa na tetesi zinazomhusishwa na kuondoka Old Traford.
  
Kiungo wa Arsenal, Granit Xhaka amewapa changamoto wachezaji wenzake kushinda taji la Europa Ligi kama zawadi ya pekee kwa Arsene Wenger, ambaye anaondoka mwishoni mwa mismu huu.

Meneja wa Chesterfield, Jack Lester ameondoka katika klabu hiyo baada ya makubaliano na uongozi wa juu.
 
Rangers wanakaribia kukamilisha dili la uhamisho wa kiungo wa Burnley, Scott Arfield. (Sky Sports)

Liverpool imeingia kwenye mbio za kuwania saini ya golikipa wa klabu ya Atletico Madrid, Jan Oblak kwa mujibu wa ripoti zilizotoka Uhispania.

Golikipa wa timu ya taifa ya Uingereza U17, Arthur Okonkwo, 16, anawindwa na RB Leipzig pamoja na Celtic kwa sababu bado hajasaini mkataba katika klabu ya Arsenal.

Golikipa wa Crystal Palace, Wayne Hennessey anatarajiwa kusaini mkataba mpya katika klabu hiyo.

Aston Villa na Crystal Palace zitashindania saini ya kiungo wa klabu ya QPR, Massimo Luongo. (Mirror)

Alexis Sanchez
Jose Mourinho hakushangilia goli la Alexis Sanchez kwenye nusu fainali ya michuano ya FA Cup kwa sababu alikuwa na ujumbe muhimu wa kiufundi aliotaka kuufikisha kwa Ashley Young na Ander Herrera.

Manchester City wanahofia kuadhibiwa na shirikisho la Soka baada ya mashabiki wa timu hiyo kuvamia uwanjani kufuatia ushindi wao wa goli 5-0 dhidi ya klabu ya Swansea Jumapili. (Star)

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anasisitiza kwamba hatatumia fedha nyingi kwa lengo la kuifukuzia Man City.

Andres Iniesta ataamua juu ya hatima yake wiki hii, huku akiendelea kuhusishwa na uhamisho kwenda China kwenye majira ya joto.

Jonjo Shelvey hatajumuishwa kwenye kikosi cha Uingereza kwenye Kombe la Dunia licha ya kiwango chake kikubwa alichokionyesha msimu huu akiwa na Newcastle.

Straika wa Aston Villa, Gabby Agbonlahor anaweza kustaafu mchezo wa soka  akiwa na umri wa miaka 31. (Sun)

Real Madrid imeripotiwa kuwa na mpango wa kumsajili Mohamed Salah kwa dau la pauni milioni 123 na mchezaji mmoja kama sehemu ya ofa. (Express)

Pep Guardiola aliwatetea mashabiki wa Manchester City kwa kuvamia uwanja wa Etihad baada ya kipenga cha mwisho, lakini alisistiza kuwa hatakuwa na pingamizi lolote kama FA itaamua kuiadhibu klabu hiyo. (Telegraph)

Rivaldo Coetzee
Rivaldo Coetzee, ambaye alikuwa anawindwa na klabu ya Celtic anaweza kulazimishwa kustaafu soka akiwa na umri wa miaka 21 kwa sababu madaktari wameshindwa kutibu tatizo la mguu wa raia huyo wa Afrika Kusini. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 23 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/23/2018 11:38:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.