Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 9 Aprili, 2018

Gareth Bale
Gareth Bale anataka kubaki Real Madrid, kwa mujibu wa mwandhishi nguli wa habari za michezo, Guillem Balague.

Fabio Capello amethitisha kuwa amestaafu kazi ya Ukocha, na kuzima uvumi ulioenea ukidai kuwa atakuwa mkufunzi wa timu ya taifa ya Italia.

Danny Welback amesema anaweza kushindania namba na Aubameyang pamoja Lacazette.

Fernando Torres ametangaza kwamba ataondoka Atletico Madrid mwishoni mwa msimu huu. (Sky Sports)

Nyota wa timu ya taifa ya Brazil, Fred anatarajiwa kutua Manchester kwenye majira ya joto - huku Man City na United zikishindana kuipata saini ya kiungo huyo wa Shakhtar Donetsk.

Manchester United 'wanamtaka Neymar kwa malipo ya Paul Pogba na Anthony Martial' kwenye dili la uhamisho na PSG.

Mbio za Arsenal kuwania saini ya nyota wa klabu ya Stevenage, Ben Wilmot zimechochewa, huku Tottenham pia ikiwa na hamu ya kumnasa.

Liverpool 'kushtukiza ofa ya mkataba wa miaka mitatu kwa Marouane Fellaini', mkataba wake na Manchester United ukielekea kuisha. (Mirror)

Arsene Wenger alipendekeza kuwa atabakia Arsenal msimu ujao, baada ya kuzungumzia mipango yake ya usajili kwenye majira ya joto.

Gary Cahill
Nahodha wa Chelsea, Gary Cahill amekiri kuwa Tottenham iko nje ya mbio za kuwania kumaliza ligi katika nafasi nne bora, huku the Blues ikiwa nyuma ya mahasimu wao wa jiji la London kwa pointi 10. (Evening Standard)

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane bado ana uhakika wa kumpiku nyota wa Liverpool, Mohamed Salah kwenye mbio za kuwania Kiatu cha Dhahabu katika Ligi Kuu ya Uingereza.

Jose Mourinho amesema Pep Guardiola anaweza kuwa alifanya makosa juu ya maoni yake aliyotoa kuhusu Paul Pogba kabla ya mechi yao. (Daily Mail)

Ander Herrera amewachukiza mashabiki wa Manchester City baada ya kipande kifupi cha video kuvuja kwenye mitandao ya kijamii kikimuonyesha kiungo huyo wa Manchester United akiitemea mate beji ya Manchester City. (Times)

Pep Guardiola anahofia Manchester City itakuwa na 
udhaifu wa kiakili kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Jumanne dhidi ya Liverpool. (Express)

Jurgen Klopp amesema kwamba Liverpool iliikataa ofa ya Manchester City ya Sehemu ya Mazoezi kwenye Ligi ya Mabingwa kwa sababu ilitolewa muda ukiwa umeisha.

Ander Herrera
Ander Herrera amekana taarifa inayodai aliitemea mate beji ya Manchester City wakati wa mchezo wao siku ya Jumamosi katika dimba la Etihad. (Telegraph)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 9 Aprili, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 9 Aprili, 2018 Reviewed by Zero Degree on 4/09/2018 11:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.