Loading...

Arsenal wako tayari kumuuza nyota huyu kwenye majira ya joto


Aaron Ramsey alijiunga na Arsenal akitokea Cardiff kwa pauni milioni 4.8 mwaka 2008 amekuwa na nafasi ya kudumu kwenye timu. Amefunga magoli 58 katika mechi 327 akiwa na klabu hiyo kwenye michuano yote.

Kiungo huyo ameshinda Taji la michuano ya FA mara tatu akiwa na Arsenal, akifunga goli la ushindi kwenye fainali ya 2014 na 2017. Amekuwa na nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha klabu hiyo msimu huu, akifunga magoli 12 na kutoa 'assist' 9 katika michezo 36 kwenye michuano yote.

Lakini kiungo huyo wa Wales anakaribia kuingia kwenye mwaka wake wa mwisho kwenye mkataba wake wa sasa na bado hajasaini mkataba mpya. Mazungumzo yamekuwa yakiendelea na wawakilishi wake lakini hakuna maendeleo yoyote.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 27 amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda Chelsea, Juventus na Manchester United kuelekea dirisha la usajili kwenye majira ya joto. Analielewa hilo na hakubali fedha maslahi madogo.

Raia huyo wa Wales ameona sehemu za makubaliano ya mkataba aliosaini Pierre-Emerick Aubameyang, Henrikh Mkhitaryan na Mesut Ozil kwenye miezi ya hivi karibuni. Pia anataka onegzeko kwwenye mshahara wake wa sasa, ambalo litamfanya awe miongoni mwa wachezaji wanaolipwa fedha nyingi katika klabu.

Aaron Ramsey
Kwa mujibu wa taarifa ya The Sun, Arsenal wako tayri kumuuza Aaron Ramsey kama hatakubali kusaini mkataba mpya kabla ya msimu ujao. Klabu hiyo haiko tayari kujiweka kwenye mazingira magumu tena kama ilivyokuwa kwa Alexis Sanchez na Mesut Ozil.

Klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Uingereza inataka kumuuza kiungo huyo kama hatasaini mkataba mpya na watahitaji angalau pauni milioni 40 kuweza kumwachia kwenye majira ya joto.
Arsenal wako tayari kumuuza nyota huyu kwenye majira ya joto Arsenal wako tayari kumuuza nyota huyu kwenye majira ya joto Reviewed by Zero Degree on 5/19/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.