Loading...

Mgombea CCM akamatwa na Takukuru


Mgombea wa nafasi ya Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kata ya Kilangala, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, Jenga Mohamedi na wajumbe saba wa Mkutano Mkuu wa kata wa chama hicho wamekamatwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) wakidaiwa kupokea na kutoa rushwa.

Akizungumza na waandishi wa habari jana Ijumaa tarehe 18 Mei, Kamanda wa Takukuru Mkoa wa Lindi, Steven Chami amesema watu nane wamekamatwa akiwamo Mgombea ukatibu aliyekutwa akitoa rushwa kwa wajumbe ili achaguliwe.

Kwa mujibu wa Chami, tukio hilo limetokea juzi saa mbili asubuhi kwenye eneo la uchaguzi huku watuhumiwa wakiwa na fedha Sh 2,000 kila mmoja huku mpambe wa mgombea huyo alikutwa na bulungutu kiasi hicho cha fedha zenye thamani ya Sh 50,000 na orodha ya majina ya wajumbe wa mkutano huo.

Alisema watuhumiwa wanashikiliwa na Taasisi hiyo hadi mahojiano yatakapo kamilika na hatua zingine za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Mgombea CCM akamatwa na Takukuru Mgombea CCM akamatwa na Takukuru Reviewed by Zero Degree on 5/19/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.