Loading...

Pluijm aliomba kuifundisha timu yetu - Azam


UONGOZI wa Azam FC umeweka bayana kuwa, kocha wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ndiye aliyeandika barua ya maombi ya kuifundisha timu yao tangu akiwa Yanga.

Pluijm ambaye ameanza kuinoa Singida United msimu huu, taarifa za uhaki­ka zinasema kuwa Mholanzi huyo ameshasaini mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Chamazi.

Akizungumza na Cham­pioni Jumatatu, Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, alisema kuwa ko­cha huyo ndiye aliyeandika barua kuwa anataka kui­fundisha klabu hiyo tangu kipindi anaifundisha Yanga.

“Pluijm yeye ndiye aliyeandika barua kuwa anatamani kuja kutufundi­sha na mara ya kwanza aliandika akiwa anaifundi­sha timu ya Yanga kwa vile amemaliza mkataba na Singida ndiyo maana watu wanamhusisha kuja kwetu ila sisi huwa hatufichi kitu kama mlivyoona kwa Ngoma (Donald), sisi huwa tunaweka vitu hadharani,” alisema Alando.
Pluijm aliomba kuifundisha timu yetu - Azam Pluijm aliomba kuifundisha timu yetu - Azam Reviewed by Zero Degree on 5/29/2018 11:20:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.