Loading...

Messi ameitaja klabu pekee anayoweza kuichezea akiondoka Barcelona

Mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi
Nyota wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya Barcelona Lionel Messi, amekanusha tetesi za kutaka kusajiliwa Manchester City na kusema hawezi kuchezea timu nyingine barani Ulaya zaidi ya Barcelona.

Messi ambaye yupo nchini Argentina kwenye kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na Fainali za Kombe la Dunia nchini Urusi, ameyasema hayo kwenye mahojiano na mtandao mmoja ambapo pia ameweka wazi mpango wake ni kuja kuichezea timu yake ya utotoni Newell's Old Boys.

"Siwezi kusaini Man City, nipo Barcelona na ndio timu pekee nitakayochezea barani Ulaya, siku zote huwa natamani kurudi kuchezea timu yangu ya Old Boys hapa nyumbani hata kwa miezi sita'', amesema Messi.

Messi mwenye miaka 30, ataiongoza Argentina kwenye fainali za mwaka huu akiwa na kumbukumbu ya kufungwa bao 1-0 na Ujerumani kwenye mchezo wa fainali katika Kombe la Dunia mwkaa 2014 nchini Argentina.

Hata hivyo Messi amesaini mkataba mpya ndani ya Barcelona ambao utamweka klabuni hapo hadi Novemba 2021. Mkataba huo una kipengele cha timu kulipa kiasi cha Euro 700 milioni, takribani shilingi Bilioni 2.
Messi ameitaja klabu pekee anayoweza kuichezea akiondoka Barcelona Messi ameitaja klabu pekee anayoweza kuichezea akiondoka Barcelona Reviewed by Zero Degree on 5/29/2018 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.