Loading...

Real Madrid wanalenga kumsajili nyota huyu wa Atletico Madrid


Real Madrid wako tayari kulipa fedha ya kuvunja mkataba wa beki wa klabu ya Atletico Madrid.

Kwa mujibu wa taarifa ya Marca, vigogo hao wa Uhispania wanatarajiwa kupambana uso kwa uso kwenye dirisha la usajili wa majira ya joto mwaka huu na wanakaribia kuipata saini ya Jose Giminez kutoka Atletico Madrid.

Beki huyo wa Uruguay kwa sasa anakadiriwa kuwa na thamani ya pauni milioni 52.3 na Real Madrid wanachukulia dau hilo kama pesa ndogo sana kwao, wakiamini kuwa ni mchezaji bora anayefaa kusajiliwa wakati huu.

Washindi hao mara 13 wa Ligi ya Mabingwa (UEFA) walikuwa na nia ya kumsajili beki huyo mwaka 2015, lakini kwa wakati ule hawakutaka kulazimisha uhamisho huo ile hali walikuwa kwenye mgogoro na Atletico na kwa hiyowakaahirisha wazo lao.

Jose Giminez
Kwa Real Madrid kumsajili Giminez wakati huu wanaweza kuwapunguzia nguvu mahasimu wao, huku wakiendelea kuimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao baada ya kufanya vibaya kwenye La Liga msimu huu.
Real Madrid wanalenga kumsajili nyota huyu wa Atletico Madrid Real Madrid wanalenga kumsajili nyota huyu wa Atletico Madrid Reviewed by Zero Degree on 5/30/2018 07:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.