Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 22 Mei, 2018

Paul Pogba
Meneja wa Juventus, Massimiliano Allegri ana hamu ya kumsajili kiungo wa Napoli, Sergej Milinkovic-Savic. Kama uhamisho huo hautawezekana, atajaribu kumrejesha Paul Pogba kutoka Manchester United. (Tuttosport)

Tottenham wamemfanya mshambuliaji wa Manchester United, Antony Martial kuwa chaguo lao la kwanza.

Nahoda wa Newcastle, Jamal Lascelles amekuwa akihusishwa na uhamisho kwenda vilabu kama Chelsea na Tottenham. (Evening Starndard)

Baada ya kuzomewa na baadhi ya mashabiki wa klabu ya Atletico Madrid wikendi hii, Antoine Griezmann anaweza kulazimisha kuondoka. (Marca)

Manchester City wanatarajia kugundua kama mkakati wao wa kusaka saini ya Jorginho wa Napoli utazaa matunda wiki ijayo.

Manchester United wana mpango wa kujaribu kwa mara nyingine tena kumnasa Gareth Bale kutoka Real Madrid. (ManchesterEveningNews)

Neymar hataondoka Paris Saint-Germain baada ya mazungumzo yake na meneja mpya wa klabu hiyo, Thomas Tuchel kuisha vizuri. (AS)

Mshambuliaji wa Tottenham, Harry Kane atakuwa nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza kwenye michuano ya Kombe la Dunia ijayo.

Santi Cazorla
Arsenal wamethibitisha kwamba, Santi Cazorla ataondoka mkataba wake utakapoisha mwezi ujao

Mshambuliaji wa Inter Milan, Mauro Icard ameachwa nje kwenye kikosi cha Argentina kitakachoshiriki Kombe la Dunia.

Eden Hazard amesema kuwa ataendelea kubaki Chelsea msimu ujao, huku akiwa na hamu ya kubeba mataji mengi akiwa Stamford Bridge.

Arsenal watamteua aliyekuwa meneja wa Paris Saint-Germain, Unai Emry kuwa meneja wao mpya wiki hii.

Meneja wa klabu ya Napoli, Maurizio Sarri anatafakari ofa aliyopewa kutoka Zenit.

PSG hawatafikiria kumuuza Kylian Mbappe hata kama watapewa ofa ya pauni bilioni 1, kwa mujibu wa rais wa klabu hiyo.

Borussia Dortmund wamemteua aliyekuwa meneja Nice, Lucien Favre kuwa meneja wao mpya.

Meneja wa Real Madrid, Zinedine Zidane amesema kuwa hawezi kubadilishana Cristiano Ronaldo kwa Mohamed Salah wa Liverpool.

Manuel Pellegrin
Manuel Pellegrin anataka wachezaji wapya watano au wanne kufanya mapinduzi kwenye safu ya mbele ya West Ham na airejeshe  klabu hiyo kwenye Ligi ya Ulaya. (Sky Sports)

Chelsea wamemfanya mshambuliaji wa Bayern Munich, Robert Lewandowski kuwa chaguo lao la kwanza kwenye usajili wa majira ya joto.

Mashabiki wa Chelsea wana wasiwasi kwamba Roman Abramovich anaweza kuondolewa katika umiliki wa klabu hiyo.

Manchester City wameanza upya mazungumzo na Leicester kumsajili Riyad Mahrez.

West Ham wamekubaliana na Manuel Pellegrini kwenye dili lenye thamani ya pauni milioni 7 kwa mwaka. (Telegraph)

Liverpool wana jaribu kumshawishi golikipa wa klabu ya AC Milan, Gianluigi Donnarumma atue Anfield.

Ipswich wamefanya mahojiano na Frank Lampard mara mbili, ikiwa ni mkakati wa kusaka meneja mpya.

Ian Wright amesema kuwa kitendo cha Arsenal kuachana na Mikel Arteta katikati ya safari ni udhalilishaji.

Danilo Pereira
Arsenal wanaendelea na nia yao ya muda mrefu kutaka kumsajili beki wa Porto, Danilo Pereira. (Mirror)

Shujaa wa klabu ya Liverpool, Terry McDermott ameziweka medali tatu za Ulaya kwenye mnada.

Aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Norwich, Grant Holt anatarajiwa kuanza maisha mpya kama mcheza mieleka. (Daily Mail)

Liverpool wameripotiwa kuwa na lengo la kuwasajili Jamaal Lascelles na James Tarkowski.

Willian ana hamu ya kubali Chelsea - lakini hatima yake itategemea kama klabu hiyo itamuuza Antonio Conte.

Klabu ya MLS, New York City inaweza kumpa Joe Hart wasaa wa kuondoka Man City kwenye majira ya joto. (Sun)

Real Madrid wanatarajiwa kuelekeza macho yao kwa Gianluigi Buffon, huku Manchester United wakisita kumuuza David De Gea.

Chelsea wako tayari kukazania ofa yao ya pauni milioni 100 kwa ajili ya usajili wa straika wa Bayern Munich, Robert Lewandowski. (Express)

James McClean
James McClean amesema kuwa Celtic ilimvunja moyo kwa kusajili mchezaji mwingine badala yake. (Record)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 22 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumanne Tarehe 22 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/22/2018 09:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.