Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 21 Mei, 2018

Jack Wilshere
Jack Wilshere ameonyesha kuwa na nia ya kusaini mkataba mpya wa miaka mitatu na Arsenal.

Jose Mourinho ataanza marekebisho ya uwanja wa Old Traford yatakayoghalimu pauni milioni 250 na zaidi kwenye majira ya joto.

West Ham watamtangaza Manuel Pellegrini kuwa mkufunzi mpya wa klabu hiyo ndani ya masaa 48 baada ya Rafa Benitez kuikataa ofa yao.

Meneja mpya wa QPR, Steve McClaren anataka kuungana na mshambuliaji wa Uskoti, Chris Martin, ambaye alifanya naye kazi katika klabu ya Derby. (Mirror)

Unai Emery ameibuka na kuwa kinara kwenye orodha ya wagombea wa nafasi ya meneja katika klabu ya Arsenal.

Jose Mourinho anadai kwamba kitendo cha Romelu Lukaku na Marouane Fellaini kutotia juhudi za kuwa fiti kuivaa Chelsea kwwenye FA Cup kimemkasirisha sana.

Manuel Pellegrini bado anaitafakari ofa ya West Ham kuwa meneja wao mpya kwa kandarasi ya miaka mitatu .

Everton watafanya mazungumzo zaidi na Marco Silva na wakala wake, Carlos Goncalves wiki hii. (Daily Mail)

Antonio Conte anaweza kufukuzwa kazi katika klabu ya Chelsea licha ya kutwaa ubingwa wa FA.

Gary Cahill ameishauri Chelsea kushughulikia hatima ya Antonio Conte mapema iwezekanavyo.

Nemanja Matic 
Nemanja Matic ameitaka Manchester United kusajili wachezaji wenye uzoefu kwenye majira ya joto. (Guardian)

Jose Mourinho ameifunga akaunti yake ya Instagram baada ya kuporomoshewa matusi kufuatia kichapo kwenye fainali ya FA.

Stoke City wanatarajiwa kujaribu tena kumshawishi Gary Rowett akubali kuinoa klabu hiyo.

Wolves wanajianda kutoa ofa ya pauni milioni 9 kumnasa kiungo wa klabu ya Rio Ave, Pele. (Sun)

Arsenal wanatarajia kumteua Mikel Arteta kuwa mkufunzi wao mpya wiki hii.

Antonio Conte ametikisa kiberiti Chelsea akiomba kufukuzwa kazi, akisema kwamba klabu hiyo imeshindwa kuendana na tamaa yake kushinda vikombe vingi na kusema kwamba hawezi kubadilisha mfumo wake wa ukufunzi au mwenendo wa maisha yake.

Manchester United wanaweza kumpoteza Marouane Fellaini, ambaye anaweza kuondoka kama mchezaji huru baada ya AC Milan kumpa ofa ya mkataba wa miaka mitatau.

David Wagner
David Wagner ameacha kupoteza muda wake kwenye ofa kutoka vilabu vingine kwa lengo la kukubali kusaini mkataba mpya wenye maslahi mazuri katika klabu ya Huddersfield. (Times)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 21 Mei, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatatu Tarehe 21 Mei, 2018 Reviewed by Zero Degree on 5/21/2018 11:50:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.