Loading...

Watu 26 wauawa katika shambulio nchini Burundi


Serikali ya Burundi inasema kuwa watu 26 wameuawa wakati wa shambulio kaskazini magharibi wa taifa hilo.

Ghasia hizo zinajiri siku kadhaa kabla ya kufanyika kwa kura ya maoni iliyokumbwa na utata ambayo huenda ikaongeza muda wa kutawala wa rais wa taifa hilo.

Kulingana na mwandishji wa BBC, waziri wa usalama nchini humo Alain Guillaume Bunyoni alisema kuwa wale waliotekeleza shambulio hilo walikuwa ni magaidi kutoka nchini jirani ya Jamhuri ya kidemokrasi ya Congo.

Walioshuhudia wanasema kuwa washambuliaji hao waliingia nyumba baada ya nyumba usiku wakiwapiga risasi watu na kuwachoma visu na kuchoma moto nyumba zao.

KUna uwezekano kwamba shambulio hilo ni jaribio la kuvuruga kura ya maoni yenye utata iliopangiwa kufanyika wiki ijayo-ikiwa ni mradi wa serikali unaoweza kumfanya rais Pierre Nkurunziza kusalia madarakani hadi 2034.

Makubaliano ya amani yaliositisha vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Burundi yamezuka upya huku makundi ya upinzani yakijipanga nje ya taifa hilo.

Huenda mgogoro wa kisiasa nchini humo ukachukua mwelekeo mpya.

Source: BBC
Watu 26 wauawa katika shambulio nchini Burundi Watu 26 wauawa katika shambulio nchini Burundi Reviewed by Zero Degree on 5/12/2018 04:35:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.