Loading...

Yanga SC wanamtaka straika wa Lipuli


Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza rasmi kutuma barua kwa uongozi wa Lipuli ukiomba kuwapatia mchezaji Adam Salamba ili kuja kikiboresha kikosi cha kwa ajili ya mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Yanga ilithibitisha jana kutuma barua hiyo ikiwa na matumaini ya kumpata mchezaji huyo ambaye amekuwa kwenye kiwango kizuri tangu msimu huu wa ligi uanze.

Salamba ambaye ni mchezaji bora wa ligi kwa mwezi Machi, ameingia kwenye rada za Yanga ikiwa inajiandaa na mechi ya ligi dhidi ya Mtibwa sambamba na ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.

Mei 16 2018 Yanga itakuwa inawakaribisha Rayon katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kucheza mchezo wake wa pili katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho, ikiwa ni baada ya kupoteza ule wa kwanza kwa idadi ya mabao 4-0 dhidi ya USM Alger ya Algeria.

Ujio wa Salamba unaweza ukaimarisha safu ya ushambuliaji ndani ya kikosi hicho haswa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho na pengine kuwa mbadala wa Donald Ngoma ambaye ana majeraha ya muda mrefu.
Yanga SC wanamtaka straika wa Lipuli Yanga SC wanamtaka straika wa Lipuli Reviewed by Zero Degree on 5/12/2018 01:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.