Loading...

Mkemi ajiuzulu baada ya Yanga kufungwa Kenya


MJUMBE wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amejiuzulu nafasi uongozi ndani ya klabu hiyo kuanzia leo. Maneno hayo ameyasema kupitia akaunti yake ya Instagram baada ya timu ya Yanga kuaga kwenye michuano ya Sportpesa Super Cup inayoendelea nchini Kenya baada ya kuchapwa mabao 3-1 na Kakamega Boys kwenye mchezo uliopigwa kwenye Dimba la Ifraha nchini Kenya.

Haya ndo maneno aliyoyasema kupitia akaunti yake ya Instagram:

Kusema Kweli Viongozi Hatukwepi Lawama Hizi 
Kwa Hakika Tumepata Aibu Kubwa Nikiwa kama Kiongozi napaswa kuwajibika kwa Hili 

Ni hatua nzuri ya kupisha Mawazo mapya kwa Wanachama wengine kuongoza Timu na Kutupeleka Mbele, pia ningependa kuwashauri Viongozi wenzangu wajitathimini na ikibidi nao waachie Ngazi Ufanye Uchaguzi Mkuu kwa Pamoja tupate Viongozi wapya kabla msimu Mpya Haujaanza 

Napenda kuomba samahani kwa wote niliowakwaza na nimesamehe wote walio nikwaza.

Naomba kutamka Rasmi Mimi Salum Mkemi
Nijaizulu nafasi zangu zote za Uongozi ndani ya Klabu yangu pendwa Young Africans Sports Club “YANGA ” kuanzia tarehe ya Leo 03/06/2018
Nawatakia kila la kheri Viongozi wenzangu waliobaki na Kuwataka Radhi tena Wanachama, Wapenzi na Mashabiki wa Yanga kwa Matokeo mabovu tuliyopata naomba tusamehane.

Nawashukuru kwa Muda mlionipa kuiongoza Klabu hii kubwa Afrika
Naomba Kuwajibika kwa Kujiuzulu
Wenu Mwanachama Mwenzenu Mtiifu
SALUM MKEMI
NIMENG’ATUKA

Mkemi ajiuzulu baada ya Yanga kufungwa Kenya Mkemi ajiuzulu baada ya Yanga kufungwa Kenya Reviewed by Zero Degree on 6/03/2018 11:07:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.