Loading...

Vigogo Serie A waikataa ofa ya Manchester City


Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza wamemfanya kiungo wa klabu ya Napoli na timu ya taifa ya Italia, Jorginho kuwa chaguo lao la kwanza kwenye dirisha hili la usajili.

Kwa mujibu wa ripoti mbalimbali, makubalino binafsi na mchezaji huyo yalikuwa yameshafikiwa, lakini bado kuna majadiliano kidogo ya kufanya.

Jorginho
Rais wa Napoli, Aurelio De Laurentiis amethibitisha kwamba waliikataa ofa kutoka kwa Mabingwa hao wa Ligi Kuu ya Uingereza.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Uingereza wameshuhudia ofa yao ya pauni milioni 43.79 kwa ajili ya Jorginho ikikataliwa.

Meneja mpya wa Napoli, Carlo Ancelotti
DeLaurentiis alisema: “Kuanzia Julai 10 hadi Julai 31, Carlo atakuwa na uwezo wa kukitathimini kikosi chote na kufanya maamuzi, Agosti 4 tutakuwa Dublin na Liverpool na tutaiona Napoli yake kwa mara ya kwanza.
“Anataka kubakiza karibu asilimia 80 ya kikosi chake cha sasa, ambayo anaona inamfaa. Malengo yetu ni golikipa, beki wa pembeni na winga.”
Vigogo Serie A waikataa ofa ya Manchester City Vigogo Serie A waikataa ofa ya Manchester City Reviewed by Zero Degree on 6/03/2018 10:52:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.