Loading...

Real Madrid yapata mrithi wa Zinedine Zidane

Rais wa klabu ya Real Madrid, Florentino Perez
Baada ya wiki kadhaa kupita tangu aliyekuwa kocha mkuu wa klabu bingwa barani Ulaya Real Madrid, Mfaransa Zinedine Zidane kuachia ngazi hatimaye timu hiyo imemtangaza kocha wa Hispania Julen Lopetegui kuziba nafasi yake.
Real Madrid imetangaza hilo jioni hii kupitia tovuti yake na kurasa zake za mitandao ya kijamii, lakini haijaweka wazi suala la mkataba ambao imesaini na mtalaam huyo wa ufundi ambaye hivi sasa yupo Urusi na kikosi cha Hispania.

Lopetegui ambaye ni golikipa wa zamani wa Hispania pia ni moja ya wachezaji waliopitia ngazi zote za klabu ya Real Madrid ikiwemo kituo cha kukuza vipaji vya soka cha timu hiyo (Castilla), kabla ya kuichezea timu ya wakubwa kwa mchezo mmoja tu na baadae kutolewa kwa mkopo.

Julen Lopetegui
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 51, pia amewahi kuwachezea mahasimu wa Real Madrid, Barcelona kwa miaka mitatu akicheza mechi 5 pekee. Lopetegui amefundisha timu za taifa za Uhispania kwa ngazi zote U17, U19, U20 na U21 kabla ya kwenda Porto FC na mwaka 2016 kuteuliwa rasmi kufundisha timu ya Hispania.
Mhispania huyo anaingia kwenye kibarua kigumu cha kuyalinda mafanikio ya Zidane ambaye ameifundisha Real Madrid kwa miaka miwili na nusu akiiwezesha kuchukua UEFA mara tatu mfululizo na La Liga moja.
Real Madrid yapata mrithi wa Zinedine Zidane Real Madrid yapata mrithi wa Zinedine Zidane Reviewed by Zero Degree on 6/12/2018 04:28:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.