Loading...

Nyota Yanga afungiwa miezi 14 kisa bangi

Mohamed Banka
Mchezaji wa klabu ya Yanga, Mohamed Issa 'Banka' amefungiwa kwa miezi 14 na Kamati ya kuzuia na kupambana na dawa zisizoruhusiwa michezoni ya Kanda ya Tano Africa (RADO) kutokana na matumizi ya dawa zisizoruhusiwa michezoni aina ya Bangi.

Disemba 9,2017 Mohamed Issa akiwa Machakos nchini Kenya alichukuliwa vipimo vya mkojo ambavyo vilisafirishwa kwenda kwenye Maabara ya WADA iliyopo Doha, nchini Qatar kwa uchunguzi.

Akitoa taarifa hiyo katika mkutano na wanahabari, Afisa Habari wa shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Cliford Ndimbo amesema kuwa mchezaji huyo alitakiwa kutoa maelezo ikiwemo kukataa au kukubali kosa ambapo Mohamed Issa alikubali mashtaka hayo kwa kukiri kosa akichagua kujitetea kwa njia ya maandishi, utetezi aliouwasilishwa August 1,2018.

"Baada ya uchunguzi wa maabara na utetezi wa Mohamed Issa,Kamati imemkuta na hatia na imemfungua kwa kipindi cha miezi 14 kuanzia Disemba 9,2018 na adhabu kumalizika Februari 8,2019", amesema.

"Wakati wote akitumikia adhabu hiyo hataruhusiwa kufanya chochote kinachohusiana na mpira wa Miguu. Hatakiwi kufanya mazoezi hadharani,hatakiwi kuonekana akishiriki", ameongeza Ndimbo.

Mchezaji huyo alitakiwa kukutana na adhabu kubwa zaidi ikiwemo kufungiwa maisha lakini kamati kwa mamlaka iliyonayo imepunguza adhabu hiyo kufikia miezi 14 baada ya kumuona Mohamed Issa ni kijana mdogo.

Aidha kamati hiyo ikijiridhisha kuwa anatumikia adhabu ipasavyo itamruhusu kuanza mazoezi na klabu yake katika miezi miwili ya mwisho katika adhabu yake.
Nyota Yanga afungiwa miezi 14 kisa bangi Nyota Yanga afungiwa miezi 14 kisa bangi Reviewed by Zero Degree on 10/31/2018 10:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.