Makonda afichua siri Dar kuongoza la 7
Alisema pamoja na Shule ya Msingi Vijibweni iliyopo Manispaa ya Kigamboni kuwa na changamoto mbalimbali ikiwemo darasa moja kuwa na wanafunzi zaidi ya 200, bado imejitahidi na kushika nafasi ya 10 kitaifa.
Baraza la Mitihani Tanzania (NACTE) lilitangaza kuwa mkoa huo, umeongoza kwa kufanya vizuri kati ya mikoa 10 bora kitaifa kiufaulu kwa kuwa na watahiniwa waliopata alama nyingi kwenye masomo matano, ukifuatiwa na Geita, Arusha, Kilimanjaro, Kagera, Mwanza, Iringa, Mtwara, Katavi na Njombe.
Akizungumza kwenye uzinduzi wa ujenzi wa ofisi za walimu shuleni Vijibweni jana, Makonda alisema mwaka 2016 alipoteuliwa kuwa mkuu wa mkoa, alipokelewa na matokeo mabaya ya darasa la saba, wakishika mkia.
Alifafanua kuwa baada ya kupata matokeo hayo, alikutana na walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari, waratibu elimu na wakaguzi wa shule ili kujadiliana changamoto wanazokumbana nazo na namna ya kuzitatua. “Tulipata changamoto kubwa 19 ikiwemo watoto kutembea umbali mrefu kwenda shule, kukosekana kwa mabweni, umeme, maji, malimbikizo na kukosekana kwa ofisi za walimu,” alisema Makonda.
Alieleza kuwa mpaka sasa shule 200 za mkoa huo, zimeshaunganishwa na umeme, na taratibu zilizopo ni kuziunganisha shule hizo na mtandao wa maji.
Aidha, alisema wana mpango wa kuchimba visima 50 ambavyo vitaunganishwa na shule, na kwa Wilaya ya Kigamboni, inapata maji kwa asilimia 42 huku visima vya Kimbiji na Mpera vina zaidi ya lita 200 za maji ambazo zitasaidia katika kuleta maendeleo zaidi.
Pia alisema jukumu lingine ambalo lilikuwa changamoto ni ofisi za walimu, ambazo zitaongeza thamani ya walimu ambao wanakaa chini ya miti na korido ili kutimiza majukumu yao.
“Ni lazima tuwape kipaumbele walimu wote kwani ndio msingi wa kazi nyingine zilizopo kwani bila walimu tusingefika tulipo. Unapoboresha mazingira ya kazi unamfanya mwalinu aone furaha kwenda shule,” alieleza.
Aliongeza, “Siwezi kukaa kwenye ofisi nzuri wakati walimu wangu wako katika mazingira mabaya. Fikiria darasa moja linabeba wanafunzi zaidi ya 200 hayo madaftari mwalimu anayaweka wapi na anayasahihishaje? Ni lazima kujenga mazingira mazuri ya walimu kwani ndio jiko letu, mpishi hawezi kupika chakula kizuri endapo mazingira yaliyopo sio mazuri.”
Makonda aliwapongeza walimu, wazazi na wanafunzi kwa kuleta matokeo mazuri kitaifa na kuwataka wadau walimu kuendekea kushikamana ili mkoa huo uendelee kushika nafasi hiyo.
Akizungumzia ujenzi wa ofisi hiyo, alisema inajengwa na Kampuni ya CRGE ya Wachina ambayo ilijenga Daraja la Mwalimu Nyerere, lengo ni kuwa na ofisi ya kisasa itakayoongeza hadhi na thamani ya mwalimu.
Alisema wataendelea kubadilisha mazingira ya walimu kwa kuwajengea vyoo binafsi ili kuepuka kubanana na wanafunzi.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Vijibweni, Huruma Mmuya alisema kati ya watoto 390 walioandikishwa kufanya mitihani ya darasa la saba (PLSE) mwaka 2018, waliofaulu ni 368 wakati matokeo ya mwaka 2017 yalionesha kuwa kati ya watoto 304 walioandikishwa, 290 pekee walifaulu kujiunga na sekondari.
Mmuya alisema shule hiyo ina wanafunzi 3,685 huku vyumba vya madarasa vilivyokuwepo ni 18 ikiwa na upungufu wa madarasa 55.
“Tuna walimu 46 na upungufu ni walimu 15, upungufu wa matundu ya vyoo 123 na madawati 70. Wadau wetu wameendelea na jitihada za kuhakikisha shule inapata madarasa mengi ambapo Ofisi ya Meya wa Dar es Salaam inajenga madarasa matano pamoja Mbunge wa Kigamboni, Faustine Ndugulile,” alibainisha Mwalimu Mmuya. Meya wa Jiji, Isaya Mwita alisema mwaka 2015-16, Shule ya Vijibweni ilikuwa na madarasa 12 ambayo darasa moja linakaa zaidi ya watoto 300, lakini kutokana na jitihada za wakazi wake wamejenga madarasa mengine.
“Madarasa matatu yanaendelea kujengwa kwani tayari matofali 4,000 yapo tayari ili kuwasaidia walimu kupunguza mlundikano wa wanafunzi kwenye darasa moja. Lakini pia walimu wetu wamekuwa kama ndege wanapokaa chini ya miti kutekeleza majukumu yao,” alieleza Mwita ambaye pia ni Diwani wa Vijibweni.
Aliomba Ofisi ya Mkuu wa Mkoa kuhakikisha inashughulikia changamoto ya upatikanaji wa eneo la Kibene linalomilikiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ili wajenge shule nyingine kupunguza wingi wa wanafunzi wanaosoma Vijibweni.
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Sarah Msafiri alipongeza shule hiyo kwa kufanya vizuri katika matokeo ya darasa la saba ambayo ilifaulu kwa asilimia 92.

Alisema sababu ya kufanya vizuri ni utashi wa kisiasa na uongozi uliotukuka, unaofanywa na Makonda na watahakikisha rekodi iliyowekwa haiwezi kuvunjwa na mikoa mingine.
Source: Habari Leo
Makonda afichua siri Dar kuongoza la 7
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2018 01:05:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2018 01:05:00 PM
Rating: