Makamu wa Rais agoma kufungua stendi ya mabasi Kibaha
Samia amefikia uamuzi huo leo Jumapili Oktoba 28, 2018 katika ziara yake mkoani Pwani mara baada ya kufika kwenye stendi hiyo na kusema hatoweza kuifungua hadi kufanyike mazungumzo baina ya viongozi wa mkoa, wilaya na wengine na kuahidi atakwenda mwenyewe.
"Dhumuni lililonileta ni kufungua stendi hii, tumepata malalamiko kidogo hivyo sitaweza kuifungua leo stendi hii, hivyo naomba mnipe wiki mbili au tatu nitakuja kuifungua.”
“Serikali ya CCM ni ya uwazi na ukweli hivyo kuna wasiwasi mdogo tu na tutaifungua, naomba shughuli zote ziendelee, napenda kumpongeza sana mkurugenzi kwa hapa mlipofikia," amesema Samia.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Kibaha, Jenifa Omolo akisoma taarifa amesema ujenzi wa stendi hiyo umegharimu zaidi Sh3.2 bilioni ambao ujenzi wake ulianza Juni mwaka jana na kwamba tangu waanze kuitumia stendi hiyo hivi karibuni imeongeza mapato ya makusanyo ya ushuru ukilinganisha na ile ya awali.
Naye Waziri wa Tamisemi, Selemani Jafo amesema ujenzi wa stendi hiyo ni wa kiwango cha juu ukilinganisha na stendi tisa zilizo kwenye mpango huo kwani umejengwa kwa kiwango cha zege ili kuhimili uzito wa magari makubwa.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo amesema kwa sasa stendi hiyo iko jirani na pori linalomilikiwa na Shirika la Elimu Kibaha jambo linaloleta changamoto hususan katika kukua kwa mji wa Kibaha.
Amesema ni vema uongozi wa Shirika la Elimu Kibaha ukaangalia uwezekano wa kuweka wawekezaji kwenye eneo hilo ili litumike na kuleta mwonekano mzuri wa mji huo.

Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2018 01:05:00 PM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
10/28/2018 01:05:00 PM
Rating: