Mwanafunzi wa kidato cha 5 ajinyonga mkoani Mwanza
Tukio hilo limetokea jana Oktoba 18, 2018 majira ya saa 12: 00 asubuhi, hii ni baada ya wanafunzi wenzake kupita eneo la uwanja wa shule kisha kuona mwili wa marehemu Ayoub aliyekuwa akisoma mchepuo wa PCB, ukiwa unaning’inia juu ya mti na kutoa taarifa kwenye uongozi wa shule ambao ulifikisha taarifa hizo kituo cha polisi.
Chanzo cha mauaji hayo bado hakijafaamika ambapo mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali ya DDH Sengerema kwa ajili ya uchunguzi pindi uchunguzi ukikamilika utakabidhiwa kwa ndugu wa marehemu kwaajili ya mazishi.
Hata hivyo, Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limesema bado wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo na kwamba linatoa wito kwa wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za uhalifu na wahalifu ili waweze kukamatwa na na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
Mwanafunzi wa kidato cha 5 ajinyonga mkoani Mwanza
Reviewed by Zero Degree
on
10/19/2018 09:35:00 AM
Rating:
