Loading...

Tanzania yapangwa na bingwa mtetezi AFCON

Maafisa wa CAF wakichezesha droo hiyo jijini Cairo Misri.
Timu ya taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Soccer Beach), ambayo imefuzu kushiriki fainali za mataifa ya Afrika (AFCON 2018), imepangwa kundi B pamoja na bingwa mtetezi Senegal.

Akiongea mapema leo Oktoba 31, 2018, wakati anataja kikosi kitakachoingia kambini kwaajili ya kujiandaa na fainali hizo, kocha wa timu hiyo Boniface Pawasa amesema wamepangwa kundi gumu lakini haiwakatishi tamaa.

''Tumepangwa kundi gumu sana ambalo lina bingwa mtetezi Senegal pamoja na Nigeria ambaye alicheza fainali na Senegal hivyo sisi tutakuwa timu ndogo kwenye kundi hilo lakini tutajiandaa kwaajili ya kushindana na kuhakikisha tunafanya vizuri'', amesema Pawasa.

Mbali na Senegal pamoja na Nigeria pia kuna timu ya Libya katika Kundi B. Kundi A lenyewe lina timu za Misri, mabingwa wa zamani Madagascar, Morocco na Ivory Coast.

Michuano hiyo itafanyika nchini Misri kuanzia Desemba 8-14, 2018 katika fukwe za mjini Sharm El Sheikh.

Wachezaji walioitwa:
  1. Ibrahim Abdallah
  2. Ahmed Juma
  3. Juma Ibrahim
  4. Roland Msonjo
  5. SAMWEL Salonge
  6. Yahya Tumbo
  7. Jarubu Juma
  8. Ahmada Ahmada
  9. Sudi Ame Sudi
  10. Alphat Ndise
  11. Kashiru Salum
  12. Musa Hassan Mgosi
  13. Ally Humud
  14. Mohamed Makame
  15. Shaffih Mussa
  16. Justine Antony
  17. Seif Mwinyi
  18. Juma Kaseja
Tanzania yapangwa na bingwa mtetezi AFCON Tanzania yapangwa na bingwa mtetezi AFCON Reviewed by Zero Degree on 10/31/2018 12:20:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.