Loading...

Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Octoba, 2018

Paul Pogba
Uhamisho wa Paul Pogba kwenda Juventus hautakuwa rahisi, huku Barcelona na PSG zikiendelea kumfuatilia Mfaransa huyo.

Chelsea inaazimia kumsajili Suso, mshambuliaji wa AC Milan mwenye umri wa miaka 24 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Italia kutoka Liverpool, mwezi Januari. (Express)

Real Madrid wataongeza mara mbili ya mshahara wa Maurcio Pochettino na kumpa ofa ya pauni milioni 17 ili ashawishike kuondoka Spurs.

Arsenal wametoa ofa ya pauni milioni 8 kumnasa nyota wa klabu ya Ajax na timu ya taifa ya Argentuina, Nicolas Tagliafico.

RB Leipzig inapania kumsajili mshambuliaji wa Everton forward Ademola Lookman, ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ujerumani kwa mkopomsimu uliyopita. Hilo litafanyika endapo kiungo huyo wa miaka 21 ataamua kuondoka Goodison Park.

Klabu ya Paris St-Germain inapania kumnunua mshambuliaji Alexis Sanchez, 29, kutoka Manchester United msimu ujao wa joto. (Sun)

Jaap Stam
Jaap Stam analenga kurejea Manchester United, huku akiitaja kazi ya umeneja kuwa kazi ya ndoto zake.

PSG wanategemea kumpoteza aidha Kylian Mbappe au Neymar wakiendeleza hitaji lao la kumsajili Alexis Sanchez. (Mirror)

Frank Lampard hatashangilia kama Derby itaifunga Chelsea kwenye uwanja wake wa Stamford Bridge michuano ya Carabao leo Jumatano.

Wachezaji wa Tottenham wanahofia huenda meneja wao Mauricio Pochettino, ambaye amehusishwa na klabu za Real Madrid na Manchester United, akaondoka klabu hiyo msimu ujao wa joto. (Telegraph)

Mkopo wa miaka miwili wa Kipa wa Liverpool Loris Karius katika klabu ya Besiktas hautavunjwa licha ya tetesi kudai klabu hiyo ya Uturuki inataka mchezaji huyo wa miaka 25 kurejea kwenye klabu hiyo ya Merseyside mwezi Januari. (Liverpool Echo)

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Michael Laudrup amekataa wito wa kuwa meneja wa klabu hiyo ya Uhispania. (AS)

Gareth Bale
Winga wa Wales, Gareth Bale, 29, ameongoza kura ya mashabiki wa Real Madrid kuhusu mchezaji aliyefanya vibaya zaidi msimu huu. (Marca)

Mshambuliaji wa Reiss Nelson, 18, ambaye yuko Hoffenheim kwa mkopo amepuuza madai kwamba huenda akaondoka klabu hiyo na kuhamia ligi ya Bundesliga nchini Ujerumani. (Independent)

Paul Mitchell ambaye ni Mkuu wa usajili na maendeleo katika klabu ya RB Leipzig, amesema hajawasiliana Manchester United kuhusu uwezekano yeye kupewa wadhifa wa mkurugenzi wa soka katika uga wa Old Trafford.

Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho anatarajia klabu hiyo imnunulie mlinzi wa kati mwezi Januari wakati dirisha la uhamisho wa washezaji litakapofunguliwa. (Manchester Evening News)
Meneja wa wa timu ya taifa ya Ubelgiji ambaye pia amewahi kuongoza klabu ya Everton Roberto Martinez anapigiwa upatu kuwa meneja mpya wa kudumu wa Real Madrid.

Neymar, 26, amesema meneja wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel alikuwa sawa kuwaacha nje ya kikosi mshambuliaji Kylian Mbappe, 19, na Adrien Rabiot, 23, wakati wa mechi dhidi ya Marseille baada ya wachezaji hao kuchelewa kufika kwa mkutano wa timu.

Juventus ina mpango wa kumsajili mchezaji wa Colombia, James Rodriguez mwezi Januari mwakani ikiwa Bayern Munich itaridhia kukatiza makubaliano ya kiungo huyo wa miaka 27 kutoka Real Madrid kwa mkopo. (Daily Mail)

Manchester United ahaitamuajiri mkurugenzi kandanda hadi pale meneja Jose Mourinho atakapoidhinisha hatua hiyo. (ESPN)
Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Octoba, 2018 Tetesi za soka barani Ulaya Jumatano Tarehe 31 Octoba, 2018 Reviewed by Zero Degree on 10/31/2018 08:05:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.