Wenger mbioni kurejea kibaruani
Kocha huyo amesema amevutiwa kurejea katika kazi yake baada ya kupata ofa za kutoka sehemu mbalimbali duniani, huku akithibitisha kuwa atafundisha katikam ngazi ya klabu.
“Ninaamini kuwa nitaanza tena kufundisha Januari mosi. Sijui hasa ni wapi nitafundisha, kwa sasa nimepumzika na nitakuwa tayari kufundisha tena”, amesema Wenger.
“Yapo pia mashirikisho ya soka, timu za taifa. Inaweza kuwa nchini Japan, nashukuru kwa miaka 22 niliyohudumu Arsenal, nimekuwa na uzoefu wa sehemu mbalimbali, hivyo ninapata mialiko dunia nzima ”, ameongeza.
Aidha, kocha huyo amezungumzia kuhusu kujiuzulu kwa Mesut Ozil katika timu ya taifa ya Ujerumani akisema kuwa hakufurahishwa na uamuzi huo kwasababu Wajerumani walikuwa wakithamini mchango wake aliokuwa akiutoa.
“ Ninapenda hasa pale wachezaji wanapokuwa katika kiwango bora. Anapoteza kitu fulani kama hachezi katika michezo ya kimataifa ”

Reviewed by Zero Degree
on
10/17/2018 05:35:00 PM
Rating: