Hatimaye Lulu amaliza kifongo chake jela
Akizungumza na wanahabari baada ya Lulu kumaliza taratibu za kifungo chake, Mkurugenzi wa Idara ya Probesheni Wizara ya Mambo ya Ndani, Aloyce Musika, leo amesema Lulu amemaliza salama na sasa ni raia huru.
Novemba 13, 2018 Lulu alihukumiwa kwenda jela miaka miwili baada ya kupatikana na hatia ya kumuua bila kukusudia, Steven Kanumba, lakini tangu Mei 14 mwaka huu, alikuwa akitumikia kifungo hicho cha nje kwa kufanya kazi za usafi katika ofisi za Wizara ya Mambo ya Ndani jijini Dar es Salaam.
“Kwa kipindi chote cha kifungo chake, Lulu amekuwa mtiifu, tumekuwa tukimfuatilia nyendo zake, tumeridhika kuwa amebadilika,” amesema Musika.
Hatimaye Lulu amaliza kifongo chake jela
Reviewed by Zero Degree
on
11/12/2018 01:50:00 PM
Rating: