Loading...

Sababu Charles Mwijage, Tizeba kutumbuliwa


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ametaja sababu ya kuwatumbua waliokuwa Mawaziri wa Kilimo, Dkt Charles Tizeba, pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage kuwa walishindwa kumaliza mgogoro wa zao la korosho.

Akizungumza wakati akiwaapisha Mawaziri wawili na Manaibu Waziri wanne Rais Magufuli alibainisha kuwa viongozi hao walishindwa kufanya maamuzi wakati wafanyabiashara wa korosho waliposhindwa kuwasimamia wanunuzi wa korosho.

"Nilimwambia Waziri Mkuu awakumbushe mawaziri wake, kwa sababu matatizo mengi yaliyokuwa yakihusu kilimo na viwanda yalikua yanamalizwa na Waziri Mkuu, nilijiuliza pia kahawa ni kilimo pia vipi Waziri hakuliona pia." Rais Magufuli.

"Nilijiuliza kwanini hawa tuliowapa ,majukumu hawafanyi hivi, ni ukweli pia bei ya soko la korosho limeshuka kidogo unapoona kuna tatizo unamtuma Waziri Mkuu anatatua," ameongeza Rais Magufuli.

"Wengine wanasema nina ubaya na majina ya kina Charles lakini labda wabadilishe majina, ila hatufanyi hivyo kwa nia mbaya, bali ni tusukume na gurudumu la maendeleo,".

Niwapongeze sana waliokuwa mawaziri wa Kilimo na Viwanda, kuwa nyinyi ni watu safi sana na ni wazalendo sana, asitokee mtu awadanganye ila hiyondio sababu ya kuwaondoa.
Sababu Charles Mwijage, Tizeba kutumbuliwa Sababu Charles Mwijage, Tizeba kutumbuliwa Reviewed by Zero Degree on 11/12/2018 01:50:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.