Loading...

Amber Rutty, mpenzi wake wakosa dhamana tena


Msanii Rutyfiya Abubakary maarufu 'Amber Ruth' na mpenzi wake Said Kitomali wamekosa dhamana tena baada ya wadhamini wao kutofika kwenye kesi inayowakabili katika Mahakama ya Kisutu Dar ya kufanya mapenzi kinyume na maumbile.

Wadhamini hao, wanatakiwa wawe na vitambulisho vya Taifa na washtakiwa hao wasalimishe hati zao za kusafiria mahakamani na wasitoke nje ya Dar es Salaam bila ruksa.

Kwa upande wa mshtakiwa mwenzao, James Delicious yeye alifanikiwa kutimiza masharti hayo ya dhamana Novemba 2, 2018 walipofikishwa mahakamani hapo kwa mara ya kwanza.

Wakili wa Serikali Mwanaamina Kombakono leo Novemba 12 katika Mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Augustine Rwizile amedai kuwa kesi ilipangwa kwa ajili ya kutajwa na upelelezi wake bado haujakamilika.

Hata hivyo, baada ya Kombakono kueleza hayo, Amber Ruty amenyoosha mkono akiwa kizimbani katika ukumbi namba 2 wa Mahakama ya wazi na kuomba dhamana.

Baada ya kutoa ombi hilo, Hakimu Rwizile ameita mahakamani hapo wadhamini wake mara kadhaa na wakili wa Serikali Kombakono naye amewaita wadhamini hao lakini hakuwepo hata mmoja.

Hivyo ameiahirisha kesi hiyo hadi Novemba 26, 2018 na kuwaeleza washtakiwa hao iwapo wadhamini wao watafika ndani ya muda wa mahakama watadhaminiwa.
Amber Rutty, mpenzi wake wakosa dhamana tena Amber Rutty, mpenzi wake wakosa dhamana tena Reviewed by Zero Degree on 11/12/2018 02:05:00 PM Rating: 5

Powered by Blogger.