Simu 897 zadakwa zikitoka Kenya
Gari hilo aina ya Probox lenye namba za usajili T 228 DGD, lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyefahamika kwa jina moja la Ngwena, likiwa ni mali ya John Makumba anayeishi Sirari.
Dereva wake aliposimamishwa na gari la askari wa doria alikaidi kusimama na kuendesha kwa kasi kwenda Kijiji cha Nkende wakifukuzana na gari la Polisi na kuharibu mazao ya watu na kutoroka. Anasakwa na Polisi.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Tarime/ Rorya, Henry Mwaibambe alisema gari hilo liligunduliwa juzi jioni katika Kijiji cha Nkende, wakati askari wa doria walipopata taarifa ya kuwepo gari lenye bidhaa za magendo kutoka nchini Kenya na walipojaribu kulisimamisha dereva wake alikaidi kusimama.
“Askari wetu walijaribu kulifuata nyuma gari hilo liliongeza mwendo kwa kasi na kutaka kugonga magari mengine kwa kukimbia na kisha kuingia barabara ya Shule ya Msingi Nkende na kuvamia mashamba ya watu na kuharibu mazao yakiwemo mahindi. Liligonga na kupasuka tairi ya mbele na kukwama kisha dereva wake kutoroka na kuingia porini na kuacha gari hilo na kukamatwa likiwa na simu hizo,” alsema Kamanda Mwaibambe.
Alisema wamejipanga kupambana na vitendo vya uhalifu vikiwemo kudhibiti biashara za magendo kwa kushirikiana na maofisa wa Mamlaka ya Mapato (TRA) katika kufanya doria katika vijiji vya mipakani vikiwemo Kogaja, Ikoma, Shirati, Kubiterere, Sirari, Gosebe Kipimo, Borega na Kegonga.
“Dereva wa gari hili kwa jina Ngwena tunamsaka kwani ni mtuhumiwa wa mara kwa mara kuhusika na biashara ya magendo ikiwemo ya dawa za kulevya na kisha kuwatoroka Polisi na mmiliki wa gari hili, John Waswa Makumba ambaye inadaiwa ni ‘clearing agent’ (wakala wa huduma za forodha) huko Sirari anatakiwa kujisalimisha mara moja kituo cha Polisi mwenyewe kabla hajakamatwa,” alieleza Kamanda.
Alisema simu hizo zitakabidhiwa kwa TRA Kituo cha Sirari ili watoe thamani ya simu hizo na maofisa wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS), nao wazikague kama zina ubora wa matumizi.

Katika hatua nyingine, Kamanda Mwaibambe alisema katika kipindi cha Januari hadi Oktoba mwaka huu, wakiwa doria usiku na mchana wamekamata pikipiki 28 zikiwa na magunia ya bangi na mirungi, huku baadhi ya watuhumiwa wakitoroka na wengine wamefikishwa mahakamani.
Source: Habari Leo
Simu 897 zadakwa zikitoka Kenya
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 04:35:00 PM
Rating: