Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Novemba, 2018
![]() |
| Cesc Fabregas |
Liverpool wana mpango wa kutoa mkataba mpya kwa Joe Gomez hata kama amebakiza miaka mitatu mkataba wake wa sasa uishe.
Raheem Sterling atalipwa pauni 300,000 kwa wiki atakaposaini kandarasi mpya na Manchester City deal.
Mshambuliaji wa Uruguay Luis Suarez, 31, anasema Barcelona hivi karibuni itaanza kumtafuta mtu atakaechukua nafasi yake licha ya kufunga hat-trick kwenye mechi ya El Clasico.
Kwa mujibu wa ripoti mbali mabli, Manchester City wanapanga kumsajili nyota wa kihispania, Pelayo Morilla. (Sun)
Chelsea huenda ikaachana na mpango wake wa kumsajili kiungo klabu ya Arsenal, Aaron Ramsey kutokana na kuimarika kwa kiwango cha Ross Barkley, na Ruben Loftus-Cheek. (Star)
Antonio Valencia ametuma ujumbe mfupi kwa Jose Mourinho, akiashiria kuwa fiti kurejea uwanjani.
Wachezaji wa Fulham watakumbana na adhabu ya kukatwa mishahara kama klabu yao itashuka daraja kutoka Ligi Kuu ya Uingereza msimu huu.
![]() |
| Aaron Ramsey |
Aaron Ramsey, 27, kiungo wa kati wa Wales, ameambiwa na Arsenal anaweza kuihama klabu hiyo msimu ujao wa joto.
Nathan Redmond wa Southampton amefungiwa kuendesha gari kwa muda wa siku 28 baada ya kukamatwa akiendesha gari kwa kasi kubwa. (Daily Mail)
Meneja wa Manchester United, Jose Mourinho ana mpango wa kufanya usajili zaidi ya moja wakati dirisha la usajili litakapo funguliwa mwezi Januari - hiyo itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kufanya hivyo katika kipindi cha miaka 10.
Meneja wa klabu ya Manchester City, Pep Guardiola anasema kuwa klabu hiyo "itafanya kila iwezalo" kumshawishi Brahim Diaz, 19 asiondoke. (Manchester Evening News)
Wanaotunga sheria za kandanda huenda wakajadili mabadiliko yatakayo fafanua sheria ya kugusa mprira kwa mkono na kuondoa "makusudi".
Nyota wa klabu ya Sevens, Luke Morgan atafanya jaribio lake la kwanza kwenye timu ya taifa ya Wales siku ya Jumamosi dhidi ya Scotland.
Kiungo wa kati wa Tottenham Dele Alli, 22, anasema "kushinda kombe sio kila kitu ukizingatia umri wangu" baada ya kutia saini mkataba mpya wa miaka sita na Spurs mapema wiki hii. (Telegraph)
Aliyekuwa nyota wa Manchester United, Jaap Stam anafuatilia kibarua cha Jose Mourinho kama "kazi ya ndoto zake".
Tottenham ina mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Watford, mfaransa Abdoulaye Doucoure, 25.
Nyota aliyesajiliwa na Liverpool kwenye majira ya joto, Fabinho anakiri kuwa mwanzo wake katika dimba la Anfield umekuwa mgumu sana. (Mirror)
![]() |
| Brahim Diaz |
Borussia Dortmund inataka kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uhispania Brahim Diaz, 19. (Metro)
Tetesi za soka barani Ulaya Ijumaa Tarehe 2 Novemba, 2018
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 07:20:00 AM
Rating:
Reviewed by Zero Degree
on
11/02/2018 07:20:00 AM
Rating:


