Loading...

Video: Mabaki ya mwili wa binadamu yapatikana katika ubalozi wa Vatican


Mabaki ya mwili wa binadamu yamepatikana katika ubalozi wa Vatican nchini Italia huku vyombo mbalimbali vya habari vikiyahusisha na binti wa kike mwenye umri wa miaka 15 ambaye amewahi kupotea mwaka 1983.

Taarifa kutoka Vatican inasema kuwa polisi wanajitahidi kubaini umri na jinsia ya mwili wa mifupa hiyo, na siku ambayo kifo kilitokea.

Vyombo vya habari vya Italia vimesema kuwa mabaki hayo huenda ni ya msichana wa miaka 15 wa mfanyakazi wa Vatican aliyepotea mwaka 1983.

Kwa mujibu wa shirika la habari la ABC, Hii leo siku ya Jumatano wanasheria wa familia ya binti huyo aliyepotea mwaka 1983 akiwa na umri wa miaka 15 wamewasisitiza waendesha mashitaka na Vatican kutoa habari zakina kuhusiana na mabaki hayo ya mifupa yaliyopatikana kwenye ubalozi huo huko Rome.

Habari hizo za kuonekana kwa mabaki hayo ya mifupa ya mwanadamu zilitangazwa jana siku ya Jumanne na kuamsha hisia za uwezekano wa kuwa mwili huo ukawa ni wa Emanuela Orlandi mtoto wa mfanyakazi wa Vatican.

Shirika la habari la ANSA limeripoti kuwa waendesha mashitaka walikuwa wakifatilia kama mabaki hayo yanaweza kuwa ni binti huyo Orlandi, ambaye alipotea Juni 22 mwaka 1983, au msichana mwingine mwenye umri wa miaka 15, Mirella Gregori, ambaye alipotea Mei 7, 1983 huko Roma.

“Tunawauliza waendesha mashitaka wa Roma kama mabaki hayo yatakuwa na mahusiano yoyote na msichana aliyepotea Emanuela Orlandi na Mirella Gregori,” mwanasheria Laura Scro amesema.

Taarifa kutoka Vatican inasema kuwa polisi wanajitahidi kubaini umri na jinsia ya mwili wa mifupa hiyo, na siku ambayo kifo kilitokea.

Video: Mabaki ya mwili wa binadamu yapatikana katika ubalozi wa Vatican Video: Mabaki ya mwili wa binadamu yapatikana katika ubalozi wa Vatican Reviewed by Zero Degree on 11/01/2018 08:35:00 AM Rating: 5

Powered by Blogger.